video ambayo imempa ushindi huo Miss Tanzania 2012, Brigite Alfred Lyimo katika shindano hilo.
Wakati warembo 131 leo wanawania taji la urembo wa Dunia (Miss World), Redds
Miss Tanzania, Brigitte Alfred Lyimo ameng’ara kwa kushinda nafasi ya
tatu katika kipengele cha Urembo wenye malengo maalum (Beauty With
Purpose).
Mrembo
huyo amewashinda warembo 129 waliwania taji hilo ambalo ni kubwa baada
ya lile la Miss World. Kilichompa ushindi mrembo huyo ni mradi wake wa
kujenga bweni la watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) ambao upo
Buhangija mkoani Shinyanga umemgharimu mrembo huyo zaidi ya sh milioni
60.
Katika
mashindano hayo, mrembo wa Nepal, Ishani Shrestha alishika nafasi ya
kwanza na ya pili ilishikwa na mrembo wa Australia, Erin Holland. Warembo wengine waliomaliza katika 10 bora ya mashindano hayo ni Noémie Happart (Ubelgiji) aliyeshika nafasi ya nne, Sancler Frantz (Brazil namba 5), Marine Lorphelin (Ufaransa) nafasi sita.
Pia
katika oridha hiyo ya washindi wapo warembo wa Ghana, Uingereza, India
na Aruba ambao walishika nafasi ya saba, nane, tisa na ya kumi.
Katika
kipengele hicho, warembo hao walifanya kazi za jamii ambazo zina
mtazamo wa kimaifa ambapo mbali ya kufanya, mrembo husika anatakiwa
kutoa maelezo ya mradi huo mbele ya majaji. Mkurugenzi wa Lino
International Agency, Hashim Lundenga alisema kuwa matokeo hayo ni
faraja kwa mashindano ya Miss Tanzania kwani yameiweka Tanzania katika
chati ya hali ya juu Duniani.
Lundenga
alisema kuwa Brigitte ambaye pia ni Miss Sinza aliweza pia kuvitangaza
vivutio vya utalii vilivyopo nchini na sura nzima ya Tanzania katika
mashindano hayo makubwa ya urembo duniani.
“Hii
ni mara ya pili kwa Tanzania kufanya vyema katika mashindano ya dunia
baada ya Nancy Sumari mwaka 2005 alipomaliza katika fainali ya warembo
tano bora kati ya warembo 120 duniani. Nancy alishinda taji la mrembo
bora wa Afrika, hivyo Brigitte ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri leo
katika fainali mashindano hayo (Miss World) yanayofanyika mjini Bali,
Indonesia, naomba tumuombee aibuke kidedea,” alisema Lundenga.
0 comments:
Post a Comment