Meneja wa bia ya Tusker Lager Sialouise Shayo akizungumza
na waandishi wa habari kwenye hoteli ya New Africa wakati wa uazinduzi
wa Tuker Project Fame 6 uliofanyika leo jijini Dar es salaam kutoka
kulia ni Aneth Kushaba Mwanamziki na mshiriki wa TPF 2010 na katikati
ni Mwanamuziki Zahir Zoro na jaji wa TPF mwaka huu .
Mwanamuziki
Zahir Zoro na jaji wa TPF mwaka huu akizungumza na waandishi wa habari
katika uzinduzi huo kulia ni Janeth Kushaba mshiriki wa Tusker Project
Fame mwaka 2010.
Meneja
Masoko wa Tusker Lager Anitha Msangi akifafanua jambo kwa waandishi wa
habari kwenye hoteli ya New Africa leo wakati wa uazinduzi wa Tuker
Project Fame 6 uliofanyika leo jijini Dar es salaam kutoka kulia ni
Aneth Kushaba Mwanamziki na mshiriki wa TPF 2010, Mwanamuziki Zahir Zoro
na Meneja wa bia ya Tusker Lager Sia Shayo.
**********
Kwa miaka 7 sasa TUSKER
PROJECT FAME imeendelea kuwapagawisha mashabiki wake Afrika Mashariki
huku ikiwa na washiriki wengi kutoka Tanzania ambao hufanya vizuri
mashindano hayo. TUSKER PROJECT FAME imerudi tena kwa kishindo na mwaka
huu ikiwa ni msimu wa 6 wenye muonekano wa kipekee kwani
mashindano haya yameboreshwa na kupanua wigo wake ambapo washindi
katika usaili wataweza kuiwakilisha Tanzania katika jukwaa la Tusker
project fame nchini Kenya, na mshindi wa mwaka huu atapata kitita cha
shilingi milioni 100.000.000 na kuingia mkataba mnono wa kurekodi kwa shilingi 200.000.000.
Akiongea
na wana habari, Meneja wa bia ya Tusker Lager Sialouise Shayo amesema
“Tunawakaribisha watanzania wote ambao wanaamini wanakipaji na wanaweza
kudhihirisha kuwa kweli wao ni nyota katika muziki. Ili waweze kujipatia
nafasi ya kushiriki watanzania wanaweza kuudhuria usaili utakaofanyika
tarehe 7 na tarehe 8 Septemba katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa
Posta jijini Dar es salaam. Vigezo na masharti vitazingatiwa na
wanachotakiwa kufanya ni kuwapagawisha majaji na kuwaonyesha kuwa kweli
mshiriki anaweza kuipeperusha bendera ya Tanzania katika mashindano”.
Mashindano
haya yatatikisa zaidi kwani Mwanamuziki mahiri Zahira Zorro atakuwa
jaji katika mashindano haya. Yeye na majaji wenzake wataanza katika
usaili. Tanzania mwaka huu itapata nafasi ya kuwakilishwa na washiriki
wenye uwezo wa kujiamini kwa hali ya juu. Mashindano hayo yataoneshwa
katika televisheni inayoongoza kwa burudani Afrika Mashariki, East
Afrika Television (EATV).
“Najivunia
na najiona mwenye bahati kuwa miongoni mwa majaji watakaohakikisha
vipaji stahiki vinang`ara na kuiwakilisha nchi yetu. Kwangu hii ni fursa
kwa kuhakikisha vipaji vipya vinaendelea kuinuliwa na nawaahidi
watanzania kusimamia haki. Ninachokiomba kutoka kwa watanzania ni
kujiamini na kuonesha vipaji vyao kwani ukweli ni kwamba vipaji tunavyo
na tunaweza.” Alisema Zahiri Zorro.
Katika
mkutano huo na wanahabari miongoni mwa washiriki wa Tusker Project Fame
miaka ya nyuma alikuwepo, Aneth Kushaba. Alisisitiza suala la kujiamini
kama nguzo ya mafanikio katika kuhakikisha mshiriki anarudi na ushindi.
0 comments:
Post a Comment