Balozi
wa Hispania nchini, Luis Manuel Ceuesta Civis (kushoto), Waziri wa
Habari, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (katikati) na
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Robin Goetzsche
wakigonganisha glasi kuashiria uzinduzi wa bia ya Castle Lager kwa klabu
ya FC Barcelona ya Hispania katika hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika
jijini Dar es salaam jana usiku.
Meneja
wa bia ya Castle Lager, Kabula Nshimo akimkabidhi Waziri wa Habari,
Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara zawadi kwenye uzinduzi
uzinduzi wa bia ya Castle Lager kwa klabu ya FC Barcelona ya Hispania
katika hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika jijini Dar es salaam jana
usiku. Wengine kwenye picha ni Balozi wa Hispania nchini, Luis Manuel
Ceuesta Civis (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL) Robin Goetzsche.
**********
Na Ibrahim Kyaruzi-Executive Solutions
Bia
ya Castle Lager imepanga kuandaa kliniki za soka ambazo zitaongozwa na
makocha kutoka Klabu ya Barcelona inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania
maarufu kama La Liga.
Hayo
yalidhibitishwa Agosti 17 mwaka huu katika Hoteli ya Hyatt jijini Dar es
Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Robin
Goetzsche wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya Castle Lager na
Klabu ya Barcelona.
Goetzsche
alisema ushirikiano huo utahusisha shughuli za soka ambazo
zitashirikisha zaidi ya timu 120 nchini kote huku wakijitahidi mradi huo
kufikia jamii katika mikoa yote.
“Kutakwepo
na kliniki za soka ambazo zitaongozwa na makocha kutoka Klabu ya
Barcelona na kuna uwezekano timu itakayoibuka bingwa katika mchezo wa
soka itakayoandaliwa na bia ya Castle kusafiri kwenda Camp Nou nchini
Hispania kucheza mechi ya kirafiki,” alisema.
Goetzsche
alisema bia ya Castle Lager imeingia mkataba wa miaka mitatu wa
ushirikiano na Klabu ya Barcelona Julai 26 mwaka huu ambapo bia hiyo
bora Afrika ndiyo mdhamini mkuu wa vigogo hao wa Ulaya na duniani barani
Afrika.
Alisema
ushirikiano huo haulengi tu biashara na wateja wao mbali jamii yote
ambayo bidhaa yao inawafikia lengo likiwa ni kukuza soka.
Mgeni
rasmi katika shughuli hiyo alikuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo, Dk. Fenella Mukangara ambaye alisifu bia ya Castle Lager kwa
kupiga hatua moja mbele kutokana na kushirikiana na Klabu ya FC
Barcelona kuendeleza soka la humu nchini.
Dk
Mukangara alisema ushirikiano huo umekuja wakati mwafaka ambao Tanzania
imekuwa ikitilia mkazo kukuza na kuendeleza vipaji vya soka katika
taasisi mbalimbali na akademi chache ambazo hazina miundombinu stahiki.
“Kwa
niaba ya Serikali ya Tanzania, napenda kuwashukuru Castle Lager kwa
kutusaidia na ninaamini hii itasaidia kuendeleza soka la humu nchini,”
alisema.
Dk
Mukangara aliongeza kuwa ushirikiano kati ya Castle Lager na Klabu ya FC
Barcelona iliyosheheni wachezaji nyota kama vile Lionel Messi, Neymar
na Andres Iniesta itakuwa changamoto katika kubadilisha maisha ya
wachezaji wa soka Tanzania.
Waziri huyo alihakikisha kufanya kazi kwa karibu na Castle Lager kuwawezesha jamii nchini kote kupitia mchezo wa soka.
“Napenda
kutoa wito kwa wanasoka wote Watanzania na wataalamu wa soka kukumbatia
fursa hii inayotolewa kwa ushirikiano wa Castle Lager na Klabu ya
Barcelona kutimiza programu zilizoainishwa kwenye mkataba kwa manufaa ya
soka letu,” alisema Dk Mukangara.
Miongoni
mwa walikwa katika uzinduzi huo walikuwa Balozi wa Hispania nchini
Tanzania, Luis Manuel Ceuesta Civis, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said
Meck Sadik, Meya wa Ilala Jerry Slaa na Mkurugenzi wa Michezo kutoka
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Leonard Thadeo.
0 comments:
Post a Comment