Nafasi Ya Matangazo

August 03, 2013

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na walimu wa kike wa Manispaa ya Sumbawanga leo tarehe 02 Agosti 2013 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga. Lengo la mkutano huo likiwa kujadili kero mbalimbali za walimu pamoja na kuzitaftia ufumbuzi. Pamoja na kero mbalimbali zilizowasilishwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alitoa maelekezo kwa Halmsahauri ya Manispaa kushughulikia kero zinazowezekana ikiwepo madai ya likizo na mengineyo. Kwa yale yaliyo nje ya uwezo wa Manispaa aliahidi kuyachukua na kuyafikisha panapohusika ili yaweze kutaftiwa ufumbuzi. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima na Kushoto ni Afsa Elimu Taaluma Mkoa wa Rukwa Bi Catherine Mashalla. 


 Katika kikao hicho walimu walitoa mapendekezo mbalimbali ikiwepo kufuta chama cha waalim (CWT) kwa madai kuwa chama hicho kimekuwa kikiwakata waalim mishahara kwa mda mrefu bila kuwa na msaada wowote kwao pindi wanapouhitaji. Mapendekezo mengine ni kupunguza idadi ya masomo kwa wanafunzi wa darasa la kwanza kutoka tisa hivi sasa na kuwawekea masomo yatakayowawezesha kusoma na kuandika kuliko hivi sasa ambapo masomo ni mengi na huwachanganya watoto. Hata hivo Mkuu wa Mkoa aliweka bayana kuwa ni vyema chama hicho kikaona ni jinsi gani ya kuwanufaisha zaidi walimu kwa kujiwekea utaratibu wa kuwakopesha au kuwasaidia kwa njia nyingine kiuchumi.
Sehemu ya waalimu waliohudhuria katika Mkutano huo katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akizungumza katika kikao hicho ambapo aliwashauri waalim kutokopa katika taasisi zisizo rasmi ambazo riba zake ni kubwa kupita kiasi. Alisema taasisi nyingi za namna hiyo zimechangia kufanya maisha ya walimu wengi kuwa magumu na badala ya kuwa msaada kwao inageuka na kuwa kero.
Mkuu wa Chuo cha Ualimu Sumbawanga Bi Witness Maeda akitoa kero mbalimbali wanazokabiliana nazo waalim ikiwepo uhaba madarasa, mabweni, bwalo na maabara chuoni hapo. Kwa ujumla kero zilizowasilishwa ziligusia mishahara hafifu ya walimu, uhaba na ubovu wa vyumba vya madarasa, kucheleweshewa madai yao ya mishahara na nauli (Salary Arears), kupandiswa madaraja na uhaba wa mafunzo ya mara kwa mara kuweza kukabiliana ni mabadiliko ya mitaala mipya. 
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa www.rukwareview.blogspot.com)
Posted by MROKI On Saturday, August 03, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo