Nafasi Ya Matangazo

August 03, 2013

 Viongozi mbalimbali wa Serikali Mkoani Mtwara Julai 25, 2013 waliungana na watazania wote katika maadhimisho ya siku ya Mashujaa iliyofanyika Mkoani humo katika Makaburi ya Mashujaa hao ambao wengi wao walishiriki Vita vya Ukombozi huko Msumbiji. 

Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Makaburi ya Naliendele, yaliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Mstaafu, Simba Kalia pamoja na wakuu wa Wilaya mbalimbali za mkoa huo, Meya na Madiwani.


Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Farida Mgomi (mbele) akipita na viongozi wenzake wa Mtwara katika makaburi hayo ya Mashujaa Naliendele.
 DC Magala wa Wilaya ya Newala akipita katika makaburi hayo ya mashujaa pamoja na viongozi wengine mbalimbali wa Mkoa wa Mtwara.
 Wakuu wa Wilaya wakipewa maelezo mbalimbali ya Mashujaa hao.
 DC wa Newala, Christopher Magala akiongozwa kuelekea katika uwanja wa maadhimisho hayo.
Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Mtwara wakifuatilia hotuba za maadhimisho hayo.
DC wa Masasi,Farida Mgomi (kushoto) akifuatilia maadhi,misho hayo kwa umakini na kushoto kwake ni DC wa Mtwara, Wilman Kapenjama Ndile akiteta jambo na DC wa Newala, Christofa Magala.
Posted by MROKI On Saturday, August 03, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo