IDARA ya Habari MAELEZO ni Moja ya Taasisi za Serikali zilizo chini ya Wizara ya Habari, vijana Utamaduni na Michezo ambayo ndio Idara yenye jukumu la kusimamia na kuratibu shughuli zote za habari za Serikali na Taasisi Zake.
MAELEZO ikiwa ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Idara ya habari inakusanya na kusambaza habari zinazohusu utekelezaji wa Shughuli za seikali na Maendeleo ya wananchi.
Pia ni Idara ambayo inahakikisha kuwa kunamawasiliano kati ya Serikali na wananchi.
Pichani Juu Afisa Habari Mwandamizi
kutoka Idara ya Habari MAELEZO, Lydya Churi akitoa bango lililo na picha za
viongozi wa Serikali na Baraza la Mawaziri kwa wananchi wa Dodoma waliotembelea
banda la Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo lililopo katika Maonesho ya
Wakulima Nane Nane Nzuguni mkoani Dodoma jana.
Lydia Churi akiwauliza maswali mbalimbali wanafunzi kabla ya kuwapa bango hilo lenye picha za viongozi.
Miongoni mwa kazi za Idara hiyo ya Habari ya Serikali ni pamoja na kupiga picha za viongozi na shughuli mbalimbali za serikali za kitaifa na kuzihifadhi, kutoa nafasi ya kumbi za Mikotano baina ya watu mbalimbali na Wanahabari.
0 comments:
Post a Comment