Kamati Kuu ya CCM Taifa itakutana tarehe 23.8.2013 ikifuatiwa na
Halmashauri Kuu keshokutwa asubuhi ambapo itakuwa kwa siku mbili.
Ajenda
Kuu ya Kamati Kuu itakuwa kujadili maoni ya wana CCM juu ya rasimu ya
Katiba, akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa White
House,Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Nape Nnauye alisema mpaka sasa CCM
na wanachama wake wameshirikiana vya kutosha kwa kuzingatia sheria na
taratibu zilizowekwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Pia Kikao hicho kitajadili hali ya kisiasa na hatma ya madiwani Bukoba na Masuala Utumishi
Alisema
siku ya Jumamosi asubuhi tarehe 24,kutakuwa na sherehe fupi za kuzindua
Baraza la Ushauri la Wazee wa CCM kabla ya kikao cha halmashauri.
Baraza hilo linaundwa na Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wastaafu wote wa CCM Taifa.
Posted by MROKI
On Thursday, August 22, 2013
No comments
0 comments:
Post a Comment