Na Jennifer Chamila, Maelezo.
MWANAMUZIKI mkongwe wa bendi ya
Msondo Ngoma Mzee Muhidin Gurumo amestaafu rasimi kazi ya muziki alioifanya kwa
muda wa miaka 53.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo Mzee Gurumo mwenye umri wa miaka 73 amesema
ameamua kustaafu kazi hiyo kwa hiari yake mwenyewe kutokana na umri wake kuwa
mkubwa.
“Muziki kwangu umekuwa kama asili
yangu na kazi yangu lakini nimeamua kustaafu kutokana na umri wangu na nitabaki
kuwa mshauri tu kwa mwanamuziki yeyote atakayetaka ushauri wangu,”alisema
Mzee Gurumo.
Pamoja na kufanya kazi ya muziki
Gurumo alisema kuwa hakupata mafanikio makubwa zaidi ya kujenga nyumba
anayoishi na familia yake.
“Mimi nimeimba kwa muda
mrefu sana lakini hata baiskeli sina,”alisema Mzee Ngurumo. Hata hivyo alisema
nashukuru kuwa ana nyumba ya kuishi na familia.
Vilevile Mzee Gurumo amewaasa vijana
kuwa wabunifu na kuupenda mziki wa zamani kwani ndio chimbuko la bongofleva na
kuwashauri wanamuziki wa sasa kuwa wavumilivu kukaa muda mrefu kwenye bendi
moja ili hata wanapoondoka mchango wao uthaminiwe.
Mzee Gurumo
ambaye ana mke na watoto wanne alisema kuwa katika maisha yake ya muziki
alifanikiwa kutunga nyimbo 60,000 na anavutiwa zaidi na mwanamziki Hussein
Jumbe na Hassani Lehan Bichuka na kwa wanamuziki wa kizazi kipya anavutiwa na
Nassibu Abdul ’Diamond’.
Mwanamuziki huyo mkongwe alianza
kufahamika katika tasnia ya muziki wa dansi kwenye miaka ya 1960 ambapo mwaka
1964 alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa bendi ya ya N
Alidumu na Mlimani Park mpaka mwaka
1985 na kuhamia Safari Sound aliyofanya nayo kazi mpaka mwaka 1990 na kujiunga
na Msondo Ngoma mpaka sasa anaamua kustaafu Muziki.
0 comments:
Post a Comment