Wakuu wa Nchi Wanachama wa
Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wamemteua Dkt. Stergomena Tax wa
Tanzania kuwa Katibu Mtendaji mpya wa Jumuia hiyo.
Wakuu hao wamemteua Dkt. Tax jioni ya leo,
Jumamosi, Agosti 17, 2013, mwishoni mwa kikao chao cha siku ya kwanza cha
mkutano wa 33 wa wakuu hao unaofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
cha Bingu wa Mutharika kwenye mji mkuu wa Malawi wa Lilongwe.
Uteuzi huo unafuatia
mapendekezo ya Baraza la Mawaziri wa SADC ambao walifanya tathmini ya wagombea
wawili wa nafasi hiyo ambako Dkt. Tax alipatiwa wastani wa alama 79 wakati
mgombea mwingine wa nafasi hiyo, Mheshimiwa Peter G. Sinon, Waziri wa
Serikali ya Shelisheli alipata alama 72.
Dkt. Tax ambaye ni Katibu Mkuu
wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki anachukua nafasi ya Dkt. Tomaz
Augusto Salamao wa Mozambique ambaye amemaliza muda wake baada ya kutumikia
nafasi hiyo kwa miaka minane.
0 comments:
Post a Comment