BIBI Siti Hamad Khamis ambaye anasumbuliwa na ugojwa wa figo ambazo
zimeshindwa kufanyakazi anaomba msaada kutoka kwa wasamaria wema
utakaomuwezesha kutibiwa.
Amelazimika kuomba msaada wa hali na mali ili kuokoa maisha yake
kutokana na gharama kubwa za matibabu zinazoendelea kuikabili familia
yake kwa muda mrefu sasa.
Kwa mfano kila wiki anatakiwa kwenda hospitali mara tatu ambapo kwa siku hulipa sh. 350,000.
Matibabu anayopatiwa ni kusafishwa damu ili kupunguza sumu mwilini, kupimwa na chanjo.
Anaomba kwa wale watakaoguswa na tatizo linalomsumbua, wamsaidie
matibau ndani na nje ya nchi au wamchangie kupitia AC 2011601674 Benki
ya NMB, tawi la Bank House.
Au wawasiliane na mumewe kwa simu 0774215217.
0 comments:
Post a Comment