MWANA dada machachari
kutoka visiwani Zanzibar ambaye ameamua kuingia katika anga ya muziki wa
Kizazi kipya, Leah Simba ameshusha mtaani wimbo wake wa kwanza na mpya unaoenda
kwa jina la Jinsi ulivyo.
Wimbo huo ambao umepigwa na midundo ya staili mpya ambayo
imetokea kushika nchini ya Kwaito umeimba na mwana dada huyo akishirikiana na
chipukizi mwingine Joseph Mwingira a.k.a
King Pozza kutoka kundi la Zeetown Sojaz kutoka Zanzibar.
Akiongea na Father Kidevu Blog, Msanii huyo Leah Simba
amesema kuwa wimbo huo amerekodiwa katika studio ya Jupiter Records chindi ya
mtayarishaji mziki Aloneym.
“Hii ni kazi yangu ya kwanza ambayo nimeifanya kwa muda
mrefu na kuhakikisha ikitoka inashika vilivyo na kunitambulisha katika anga ya
bongo fleva Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania, nikiwa nimesmhirikisha King
Pozza ambao nao kupitia kundi lao ndio kwanza wameachia wimbo wao wa
Chinjachinja,” alisema Leah.
Aidha Leah amesema kuwa anataraji kufanya kazi nyingi zaidi
za mziki hivyo anaomba saport ya mashabiki maana mziki ni kazi nayeye ameamua
kuifanya kazi hiyo kwanguvu na uwezo wake wote.
“Mziki ni Kazi name nimeamua kuifanya hivyo nataraji mengi
sana kupitia mziki na mashabiki wa tasnia hii ya burudani nao wakae mkao wakula
nimekuja kuwapa burudani ili name nipate kipato kupitia kazi hii,” alisema
Leah.
Leah amesema niimani yake kuwa lengo lake la kufika levo za
juu ambazo wamefikia wasanii wakubwa wa hasa wa kike katika mziki zitatimia
endapo kazi yake hiyo itapata mashabiki wengi.
0 comments:
Post a Comment