Nafasi Ya Matangazo

July 02, 2013

Rais Barack Obama wa Marekani ameondoka nchini mchana huu kurudi nchini Marekani,baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini iliyoanza jana.Rais Obama na mwenyezi wake Rais Jakaka Kikwete,leo walifanya ziara ya kutembelea mitambo ya kuzalisha umeme ya Symbion iliopo Ubungo jijini Dar es Salaam na kuzindua rasmi mradi huo.
 Rais wa Marekani Barack Obama ameweka mauwa kwenye makaburi ya waathiriwa wa mashambulizi ya mabomu dhidi ya ubalozi wa Marekani nchini Tanzania mwaka 1998, kama ishara ya kuwakumbuka.

Raia 11 wamarekani waliuawa katika shambulizi hilo lililofanywa na kundi la kigaidi la al-Qaeda ambaklo lilifanyika wakati mmoja na shambulizi lililofanywa dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Nairobi, Kenya.
Obama aliuungana na rais mstaafu wa Marekani George W Bush kwa kumbukumbu hizo.

Rais Obama yuko katika mkondo wa mwisho wa ziara yake ya pili ya Afrika akiwa rais , ambapo alitembelea Senegal na Afrika Kusini.

Aidha Obama pia atamtembelea kituo cha kuzalishha umeme kinachomilikiwa na Marekani nchini humo, kufuatia tangazo lake mwishoni mwa wiki la mradi wa umeme utakaogharimu mabilioni ya dola.

Mradi huo wa miaka mitano, unatarajiwa kusaidia kuongeza kasi ya uzalishaji wa umeme kusini mwa jangwa la Sahara,kwa ushirikiano na mataifa ya kiafrika pamoja na sekta binafsi.

Akiwa nchini humo, Obama pia anatarajiwa kuzindua mpango unaonuia kusaidia nchi za Afrika Mashariki ikiwemo, Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda kushirikiana kibiashara.

Wakati huohuo, mkewe Obama, Michelle anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa wake za marais, unaoandaliwa na taasisi ya George W Bush huku ukiongozwa na mkewe Laura Bush. SOURCE: BBC
Posted by MROKI On Tuesday, July 02, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo