Nafasi Ya Matangazo

July 02, 2013



  Meneja muendeshaji wa kanda ya Dar es Salaam kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti Joseph Silumbe(kushoto) na Meneja mauzo wa eneo Benson Bwanga wakikabidhi mfano wa hudi ya shilingi milioni 1 kwa mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushinde Michael Mbuya, 29,(kulia) mwishoni mwa wiki katika hafla iliyofanyika New Mashilingi Bar iliopo Tabata- Kisukuru jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushindeinayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti, Mwl. Michael Mbuya, akiongea na vyombo vya habari mwishoni mwa wiki mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi milioni 1katika bar aliyopatia kizibo cha ushindi New Mashilingi Bar iliopo Tabata- Kisukuru jijini Dar es Salaam.

Akiendelea kujipongeza kwa kunywa Serengeti baridi, Mshindi wa droo ya pili ya Winda na Ushinde inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti, Mwl. Michael Mbuya wakati wa hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 1 kwa mshindi huyo tabata jijini Dar es Salaam.

30 Juni 2013, kufuatia kuchezweshwa kwa droo ya pili na kutangazwa kwa mshindi wa promosheni ya Winda na Ushinde bwana MICHAEL VARELIAN MBUYA (29) ambae ni mwalimu wa shule ya sekondari ya Magoza mkazi wa Tabata jijini Dar es salaam uliofanyika katika ofisi za kampuni ya bia ya Serengeti jijini Dar es salaam. Mshindi huyo amekabidhiwa rasmi kitita hicho na kampuni ya bia ya Bia ya Serengeti ambapo zoezi hilo lilifanyika Tabata katika baa ya New Mashilingi Bar jirani na makazi ya mshindi huyo.

Kwa shangwe kubwa bwana MICHAEL MBUYA alipokea pesa hiyo na kusema “Nina furaha isiyokifani kuwa mshindi wa promosheni hii na nilikuwa nikisubiri kwa hamu pesa zangu.

Nawshukuru kampuni ya bia ya Serengeti kwa uaminifu mkubwa na kutimiza ahadi yao. Pia nawapongeza kwa promosheni hii ya Winda na Ushinde, na mbali na ushindi huu mkubwa tayari nimeshajindia bia nyingi za bure na pesa taslimu ambazo huwa natumiwa kupitia M pesa. Naahidi kuendelea kushiriki mashindano haya kwani bia ya Serengeti ndio bia niipendayo na nawapongeza sana kampuni ya Serengeti kwa kuanzisha mashindayo haya” alisema mshindi huyo.

Akiongelea promosheni hii Meneja Mauzo wa kampuni ya bia ya Serengeti  eneo la Tabata bwana Benson Bwanga  alisema “promosheni hii ni ya kipekee na mpaka sasa watu zaidi ya 11000 wameshajishindia bia za bure na pesa taslimu ambazo ni shilingi 10,000 na100,000 na wateja wetu wataweza kujishindia zaidi ya milioni moja kwa kizibo kimoja tu cha bia ya Serengeti na kuyabalisha maisha yao.”
 Akikabidhi zawadi kwa mshindi Meneja Mwendeshaji wa kanda bwana Joseph Silumbe alisema “Lengo la kampuni yetu ni kuendeleza umoja na mshikamano  na wateja wetu kwa kuutambua na kuuthamini mchango wa wateja wetu kwani wao ni muhimili mkubwa katika kukuza na kuendeleza bai yetu ya Serengeti. Na sasa kampuni ya Serengeti inachezesha promosheni hii kutimiza azma yake ya kuinua uchumi wa wateja wao kama sehemu ya shukrani kwa wateja wetu”

Ni wakati wako ndugu mteja kushiriki mara nyingi uwezavyo na kuhakikisha unajishindia zaidi ya milioni saba. Ili kushiriki unatakiwa kufungua chini ya kizibo cha bia ya Serengeti na utakuta namba maalumu na unatakiwa kuituma kwenda namba 15317 na utapokea majibu.
Tafadhari kunywa kistaarabu na ni maalum kwa 18+
Posted by MROKI On Tuesday, July 02, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo