Nafasi Ya Matangazo

July 23, 2013

 Meneja Mawasiliano na Huduma za Jamii wa Benki ya Barclays Tanzania, Tunu Kavishe (kushoto) akikabidhi mfano wa hundi yenye thamaniya shilingi Milioni 120 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Nkwamira, Nooreen Mazalla (kulia) kwaajili ya kusaidia vijana waishio mtaani bila elimu au kazi, makabidhiano hayo yalifanyika Dar es Dar es salaam jana. Wengine pichani ni Meneja Miradi wa Nkwamira, Alice Mwiru pamoja na Mtaalam wa masula ya Ufundi, David Bavo.

 Meneja Mawasiliano na Huduma za Jamii wa Benki ya Barclays Tanzania, Tunu Kavishe (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kukabidhi  hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 120 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Nkwamira Sustainable life Trust, Nooreen Mazalla (kulia) kwaajili ya kusaidia vijana waishio mtaani bila elimu au kazi. Kushoto ni Meneja Miradi wa Nkwamira, Alice Mwiru .
 Meneja Mawasiliano na Huduma za Jamii wa Benki ya Barclays Tanzania, Tunu Kavishe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya mpango huo ambao utawashirikisha vijana 60 kutoka Dar es Salaam na 40 kutoka Morogoro.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Nkwamira Sustainable life Trust, Nooreen Mazalla akieleza kuwa msaada huo kutoka Barclays Benki Tanzania kwaajili ya kuendeleza vijana ni mkubwa na utaenda mbali sana kuwasaidia vijana hao, na kuahidi kuuendeleza na kupata vijana hao hadi watakapo patikana washindi wawili. 
Barclays kupitia mpango wa kusaidia jamii unangalia vijana waishio mitaani wasiokuwa na uwezo wa kujiendeleza kielimu au kupata kazi kutokana na kutokuwa na elimu.  Aidha Noreen Mazalla amesema kuwa vijana watakaofaidika katika mpango huo ni wale walio na umri kati ya miaka 15 - 35 ambao watapata nafasi ya kujiendele\za kwa kuwapatia mafunzo ambayo yatagusa mada za kuendesha biashara zao pamoja na mafunzo ya kifedha.
Posted by MROKI On Tuesday, July 23, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo