NA JENNIFER CHAMILA- MAELEZO
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya
Kikwete amemteua Balozi Matern Lumbanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya Mamlaka ya Manunuzi Serikalini ( PPRA).
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo
vya habari na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya PPRA
Laurent Shirima imeeleza kwamba uteuzi huo , umeanza rasmi
kuanzia Juni 20 ,mwaka huu ambapo Balozi Lumbanga amechukua nafasi
ya Dk. Enos Bukuku aliyemaliza muda wake katika uongozi huo.
Taarifa hiyo ilifafanua kuwa Balozi Lumbanga ni
mchumi kitaaluma,ana Shahada ya kwanza ya Uchumi ambayo ameipata katika Chuo
Kikuu cha Dares salaam(UDSM).
Pia ana Shahada ya Uzamili pamoja na Shahada ya
Uzamivu katika masuala ya Mahusiano ya Kimataifa taaluma aliyoipata chuo
cha Geneva School of Dipmacy and International Relations, Switzerland.
Balozi Lumbanga ameitumikia Serikali ya Tanzania
katika nyazifa mbalimbali tangu mwaka 1972,mwaka 1995 aliteuliwa kuwa Katibu
Mkuu Kiongozi nafasi alioishika hadi mwaka 2006 alipoteuliwa kuwa Mwakilishi wa
Kudumu wa Tanzania katika ofisi za Umoja wa Mataifa (UN) nchini
Geneva.Amestaafu utumishi wa umma Julai mwaka jana (2012).
Balozi Lumbanga amekuwa
Mwenyekiti wa tatu wa bodi ya PPRA tangu ilipoanzishwa mwaka 2005 ambapo
Mwenyekiti wa kwanza alikuwa Bw.Philemon Luhajo na kufuatiwa na Dk.Bukuku.
0 comments:
Post a Comment