Dk. Mwelecele Malecela-Mkurugenzi wa NIMR
Hussein
Makame –MAELEZO
SERIKALI
imewaomba wananchi wa mikoa ya Dar es Salaam na Mwanza wenye umri kuanzia miaka
mitano na kuendelea kujitokeza kwa wingi katika zoezi la umezaji wa dawa za
Matende na Mabusha(Ngirimaji),na Kichocho
litakalofanyika kuanzia Juni 22 hadi na Agosti mwaka huu.
Wito huo
umetolewa na Afisa Mradi wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Magonjwa
Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele (NTD), Bernad Kilembe katika mafunzo kwa
Wahariri wa Vyombo vya Habari juu ya mpango huo yaliyofanyika ofisi za NIMR jijini Dar es
Salaam leo.
Alisema zoezi
hilo linatarajiwa kufanyika katika majiji
hayo kuanzia Juni 22 hadi 26 mwaka huu na litakuwahusisha wakazi
wote wa maeneo hayo, ambapo watameza dawa za ALBENDAZOLE na MECTIZAN kwa Dar es
Salaam na PRAZIQUANTEL kwa Mwanza.
Alisema zoezi
hilo litafanyika katika vituo 1500 vilivyoko jijini Dar es Salaam ambapo kwa
upande wa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano watameza dawa ya PRAZIQUANTEL
kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa kichocho.
Alivitaja vituo
hivyo kuwa ni shule za msingi, vituo vya mabasi,sokoni, magerezani, taasisi
mbalimbali, maofisini na kambi za jeshi.
Alisisitiza
kuwa kwa upande wa watoto wanatakiwa wameze dawa ya PRAZIQUANTEL masaa mawili
baada ya kula, ambapo kwa mkoa wa Mwanza zoezi litahusisha umezaji wa dawa hiyo
kwenye shule za msingi kwa watoto wenye umri wa kwenda shule za msingi mwezi wa
Agosti, mwaka huu.
Akizungumzia
ugonjwa Matende na Mabusha,Kilembe alisema maambukizi ya magonjwa hayo na
kichochco yameenea karibu nchi nzima ambapo alisema tatizo hilo lipo kwa
kiwango cha kuanzia asilimia 1 hadi 69.
Akizungumzia
zoezi hilo, Afisa Mradi wa NTD, Dk.Edward Kirumbi aliwataka wananchi wa majiji
hayo kuondoa hofu juu ya dawa hizo kwa kuwa hazina athari huku akikanusha uvumi
kuwa ukipasuliwa ngirimaji utakufa au itaathiri nguvu za kiume.
Naye Mkurugenzi
wa Kinga kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Neema Rusaibamayila
aliwataka wahariri hao kufikisha ujumbe kwa jamii na kuwahamasiaha wananchi
kuhudhuria kwenye zoezi hilo.
Mpango huo unahusisha
udhibiti wa magonjwa matano ,ambayo ni Matende na Mabusha(Ngirimaji), Magonjwa mengine
ni Usubi, Trakoma na Minyoo ya Tumbo.
Alisema ugonjwa wa
Matende na Mabusha husababishwa na minyoo midogo,huenezwa na mbu aina ya
Culex na Anopheles, wakati ugonjwa wa kichocho husababishwa na minyoo jamii ya Schistosoma.
0 comments:
Post a Comment