USAJILI
wa timu za mikoa inayoshiriki mashindano ya soka ya vijana chini ya
umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mwaka huu umekuwa na mwitikio
mkubwa miongoni mwa vijana wa umri huo katika mikoa ya Temeke, Ilala,
Kinondoni na Tanga.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti makatibu wa mikoa hiyo ambao ndiyo wanaoratibu
zoezi hilo la usajili wamesema kuwa vijana wengi wamejitokeza kiasi cha
kulazimika kufanya mchujo ili kupata timu sita zinazotakiwa kushiriki
Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa.
Katibu
wa mkoa wa kisoka wa Temeke, Mbarouk Mohamed alisema jana jijini Dar es
Salaam kuwa kumekuwa na mwitikio wa ajabu ambapo zaidi ya timu mia
zimejitokeza na kuwalazimu kuanza kufanya mchujo kwa kuzingatia vipaji
ili kupata idadi ya timu sita zinazohitajika kushiriki.
“Kwa
kweli ni vijana wengi mno wanaotaka kushiriki mashindano haya ya Airtel
Rising Stars na tunaamini kuwa kujitokeza kwao kwa wingi kunatupa wigo
mpana wa kupata wachezaji wazuri watakao tuwezesha kutetea ubingwa wetu
katika fainali za ARS Taifa”
Naye
Katibu wa Mkoa wa Ilala, Kanuti Daudi alisema kuwa mchakato usajili
unaendelea vizuri na vijana wengi kujitokeza kwenda kujisajili.
“Kutokana mwitikio huu tunatarajiza kumaliza usajili mapema kabla ya
muda wa mwisho uliowekwa ambao ni Juni 11, 2013”, alisema Daudi.
Kwa
upande wake Katibu wa Mkoa wa kisoka wa Kinondoni, Isack Mazwile
alisema kuwa wameanza rasmi zoezi la usajili Jumapili iliyopita na
kulingana na mwitikio wa vijana wengi wanatarajia kukamilisha zoezi hilo
wiki hii. “Tutalazimika kufanya mchujo ili kupata vijana wenye vipaji
vya soka wataounda timu sita za mkoa wetu”
Mkoa
wa Tanga unaoshirikisha timu za wasichana pekee umeanza kuendesha ligi
ambayo ndiyo inayotumika kubaini wachezaji wenye vipaji na hatimaye
kuunda timu sita kwa ajili ya Airtel Rising Stars mkoani humo.
“Sisi
huku tumeshaanza mchakato wa kutafuta timu kwa upande wa wasichana , na
kwakweli nimefurahi kuona mwitikio wa timu umekuwa mkubwa na hapa
tunajiandaa kuzichuja ili tuweze kupata timu bora, “ alisema katibu wa
soka mkoa wa Tanga Beatrice Shabani.
Mbali
na mkoa wa Tanga mikoa mingine inayoshirikisha wasichana pekee ni
Kigoma na Ruvuma wakati mikoa ya kisoka ya Kinondoni, Ilala na Temeke
inashirikisha wavulana na wasichana huku Morogoro, Mwanza na Mbeya
ikijumuisha wavulana pekee.
Mikoa
ya Morogoro, Mwanza, Kigoma, Ruvuma na Mbeya pia imeshaanza usajili na
inatarajia kukamilisha zoezi hilo kabla ya siku ya mwisho Juni 11.
0 comments:
Post a Comment