Nafasi Ya Matangazo

February 10, 2026



Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi amesema kuwa Serikali inatambua jitihada za wabunifu wa nyenzo mbalimbali zinazosaidia kupunguza gesijoto inayotokana na matumizi ya mafuta kwenye vyombo vya moto.
 
Amesema hayo wakati mkutano na wadau kutoka Jumuiya ya Vyombo vya Moto vitumiavyo Umeme Tanzania (TAEMA) pamoja na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujadiliana na kuweka mikakati ya namna bora ya kuifanyia huduma hiyo iwe endelevu.
 
Dkt. Muyungi alitoa wito kwa wadau hao kuendelea kuongeza wigo wa huduma ya usafirishaji kwa kutumia magari ya umeme kwa kuwa hivi sasa Tanzania imeanza kuzalisha umeme wa kutosha hususan kutoka Bwawa la Nyerere. 
 
“Tunawahitaji sana ninyi wadau wa sekta hii ya usafirishaji wa vyombo vya moto vya umeme, mtumie fursa ya upatikanaji wa umeme wa uhakika kwani mtasaidia katika kupunguza uzalishaji wa gesijoto,” alisisitiza.
 
Aidha, Dkt. Muyungi alipongeza mchango wa COSTECH katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi hususan kupitia tafiti zake ikiwemo Programu ya Utafiti wa Mabadiliko ya Tabianchi.
 
Pamoja na hayo alitoa wito kwa Tume hiyo kuwekeza kwenye teknolojia ya kukabiliana na maabdiliko ya tabianchi kuhakikisha inakuwa chanzo cha maarifa ya kukabiliana na changamoto hiyo.
Posted by MROKI On Tuesday, February 10, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo