Nafasi Ya Matangazo

February 11, 2026







Mtuhumiwa wa makosa nane ya kikodi Bw. Matondo Kilugala Malanda, mmiliki wa kampuni ya Matondo Breweries Investment Limited, iliyopo Wilaya ya Bukombe amefikishwa katika Mahakama Kuu mkoani Geita na kusomewa mashtaka nane ya kikodi yanayomkabili.

Mtuhumiwa huyo alifikishwa mbele ya Mahakama kuu Geita tarehe 10 Februari, 2026, ambapo shauri lake lilisikilizwa  na hakimu Mkazi Mhe. Cleofas Waane.

Akizungumza kuhusu shauri hilo, Wakili wa Serikali Bw. Emmanuel Cheneko amesema mtuhumiwa huyo anakabiliwa na makosa nane ya kikodi, ikiwemo kuanza uzalishaji bila kuwa na leseni halali, matumizi ya stempu bandia, kukutwa na bidhaa zinazopaswa kulipiwa ushuru wa bidhaa bila kulipiwa ushuru huo, pamoja na kushindwa kuandaa na kuwasilisha ritani za ushuru wa bidhaa kama inavyotakiwa kisheria.

Aidha, Meneja wa Idara ya Upelelezi wa Kodi Kanda ya Ziwa, Bw. Joel Mbilinyi, amewakumbusha wazalishaji wa pombe kali kuwa pamoja na kupata usajili kutoka BRELA, wanapaswa pia kupata leseni ya uzalishaji kutoka TRA kwa mujibu wa sheria, ili kuepuka kuchukuliwa hatua za kisheria.
Posted by MROKI On Wednesday, February 11, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo