Haijawai kutokea mpambano mkali katika GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE
kama uliooneshwa jana katika fainali za mchuano
Pan-African Guinness Football Challenge kupitia televisheni za ITV na Clouds TV .
Fainaili ilikuwa na ushindani mkubwa
ambapo timu mbili kutoka Afrika Mashariki na nyingine mbili kutoka
Afrika Magharibi zilichuana vikali kila timu zikiwania kupeleka ushindi nchini
kwao. Ilikuwa ni zaidi ya kupeperusha bendera ya Kenya kwani nchi zote za
Afrika Mashariki ziliwakilishwa na timu hiyo.
Mchuano huo ulianza kwa shangwe katika raundi ya maswali na majibu
ambapo Ephantus na Samuel kutoka Kenya walingara. Raundi ya kwanza iliisha timu
moja kutoka Kenya ikiwa inaongoza na timu nyingine kutoka Kenya ikishika mkia,
Francis na Kepha kutoka Kenya walikuwa wa kwanza kutolewa wakijishindia dola za
kimarekani 4,500 tangu washiriki mashindano hayo.
Wakiwa na presha kubwa timu
moja kutoka Afrika Mashariki iliyobakia (Ephantus na Samuel) ilionesha jitihada
zake kubwa za kutowaangusha wana Afrika mashariki kwani walijua fika kwamba si
Kenya pekee inayowategemea bali Tanzania na Uganda zimeelekeza macho yao katika
timu hiyo.
Kuelekea katika raundi ya pili, je timu mbili kutoka Ghana
zitaifungisha virago timu ya Kenya na kuifanya Afrika Magharibi kuingiiza timu
zote katika hatua inayofata? Akiwa katika jezi ya bluu Jonathan kutoka Ghana
alimudu maswali lakini kwa mara nyingine timu kutoka Kenya ilimkabili
vyema na kurudisha mashambulizi. Mwisho wa mchuano wa raundi hiyo Jonathan na
Desmond kutoka Ghana waliaga mashindano
wakiwa na kitita cha dola 25,000.
Bara liligawanishwa vilivyo baada ya timu ya Kenya (Ephantus na
Samuel) kutoka Afrika Mashariki na timu ya Ghana (Emmanuel na Isaac) kutoka
Afrika Magharibi kuingia katika hatua ya penati. Timu hizi zilikutana wiki
iliyopita katika nusu fainali na sasa ni timu ipi itatwaa ushindi na
kuipeperusha bendera ya nchi yake?
Pamoja na kushindwa wiki iliyopita, Ephantus na Samuel kutoka Kenya
kwa ujasiri mkubwa na uwezo mkubwa waliouonesha jana waliweza kuwashinda
waghana na kujipatia nafasi ya kufika hatua ya ukuta wa pesa wa Guinness.
Emmanuel na Isaac kutoka Ghana waliikosa nafasi ya ukuta wa pesa wa
Guinness ila waliondoka kwa furaha huku
wakijivunia kuwa timu bora kutoka Afrika Magharibi huku wakiwa na kitita cha dola za
kimarekani 9,000 mfukoni.
Ephantus na Samuel walithibitisha uwezo wao kwa kupiga `target four’
katika ukuta wa pesa wa Guinness na
kuwafanya wajishindie dola za kimarekani 12,000.
“Kampuni ya bia ya Serengeti inatoa pongezi kubwa kwa Ephantus na
Samuel! Kwani hawakuipeperusha bendera
ya Kenya pekee bali wameiwakilisha
Afrika Mashariki kwa ujumla. Hongereni
sana! Tumekuwa tukitazama mashindano haya kwa wiki 12 kupitia televisheni za
ITV na Clouds TV na tumeona timu
mbalimbali kutoka Afrika zikichuana kuwania ushindi wa GUINNES FOOTBALL
CHALLENGE lakini kwa uwezo mkubwa
waliotuonesha, ushindi umebaki kwetu Afrika mashariki “. alisema Meneja wa bia
ya Guinness Davis Kambi.
Mashabiki wetu wanaweza kuendelea kushiriki mchezo huu wa GUINNESS
FOOTBALL CHALLENGE kupitia simu zao na kujipima uwezo wao katika mchezo huu.
Jiunge bure kupitia m.guinnessvip.com na uone uwezo wako katika kuiwakilisha
nchi yako.
Hakikisha unatembelea ukurasa
wetu wa Facebook
Tafadhali
kunywa kistaarabu. Ni maalumu kwa 18+
0 comments:
Post a Comment