Na Mwandishi wetu
TIMU inayoundwa na wachezaji kutoka vyombo vya
habari mbali mbali vilivyoshiriki katika michuano ya NSSF “NSSF Media All
Stars” imevunja mwiko wa timu ya Bunge FC ya kutofungwa kwa miaka tisa baada ya
kuichapa kwa bao 1-0.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa
Jamhuri na kuhudhuliwa na watazamaji wengi katika historia ya uwanja wa
Jamhuri, ulikuwa mkali na wa kusisimua na timu zote zilishambuliana kwa zamu.
NSSF All Media ilianza mchezo huo kwa kasi
kufanya mashambulizi makali katika dakika 10 za kwanza. Julius Kihampa alikosa
bao la wazi katika dakika ya pili baada ya pasi safi kutoka kwa Mbozi
Katala ambaye alishirikiana vyema na Maulid Kitenge, Wilbert Molandi na
Emmanuel China.
Dakika ya saba, shuti la faulo iliyopigwa na
nahodha wa timu hiyo, Majuto “Ronaldo” Omary iligonga mwamba baada ya kumshinda
kipa wa Bunge FC Idd Azzan ambaye hakuweza kufanya lolote.
NSSF All Media ilisheherekea bao lake pekee
katika dakika ya tisa kwa kichwa kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Majuto
ambaye aliwatoka walinzi wawili kutoka upande wa kulia na kupiga krisi safi.
Bunge FC ilijikuta ikiutafuta mpira kwa
tochi muda mwingi, ilishindwa kufanya mashambulizi ya kina karibu dakika
70 na kuifanya NSSF All Media Stars iliyokuwa chini ya kocha wake, mchezaji wa
zamani wa mabingwa wa soka nchini Yanga, Sanifu Lazaro ilitawala muda
mwingi.
Baada ya goli hilo Bunge FC walijitahidi
kushambulia lakini ngome ya NSSF Media Cup Stars FC chini ya kipa Said Ambua
ilikuwa imara kuokoa hatari zote langoni.
Katika mechi ya wanawake, Bunge Quuens
iliyokuwa ikiongozwa na Halima Mdee (GK) na Esta Bulaya (WD) ilitoka kifua
mbele kwa magoli 31 kwa 18 ya NSSF Media Cup Stars Queens.
Katika mechi hiyo iliyoshuhudiwa na mawaziri
mbalimbali pamoja na huku mgeni rasmi akiwa pamoja na Naibu Spika
wa Bunge. Bunge Queens ilikuwa ikiongoza kwa magoli 17-10.
Magoli ya NSSF Media Cup Stars Queens
yalifungwa na Lulu Habib na Imani Makongoro (GS) aliyemtoa jasho halima Mdee
(GK).
Baada ya mechi hiyo Naibu Spika, Job
Ndugai alizipongeza timu za kombaini za NSSF hasa ya soka ambayo imeweka
rekodi mpya kwa kuwafunga wabunge kwenye uwanja wao.
“ Mmeonyesha uwezo mzuri lakini pia mmeonyesha
kweli nyie ni wachezaji makini kwani mara kwa mara wabunge hawafungwi hapa
Dodoma lakini nyinyi mmekuwa wa kwanza hongereni sana," alisema Ndungai
ambaye ndiye alikabidhi vikombe kwa washindi kwa kushirikiana na Mkurugenzi
Mkuu wa NSSF, DK Ramadhan Dau.
Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Venance Mwamoto akiwa na Kombe pamoja na wachezaji wa NSS Media Allstar.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dr. Ramadhan Dau akiwa na vikombe vya NSSF Media Allstar
Kikosi kamili cha Nssf Media Allstar katika picha ya pamoja.
0 comments:
Post a Comment