Nafasi Ya Matangazo

May 20, 2013

 Kikosi cha Taswa Fc, TIMU ya Taswa Fc jana iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya Full Mabondia, inayoundwa na mabondia mahiri wa Jijini Dar es Salaam. Timu hizo zilikutana katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar jana mchana, huku timu ya mabondia ikiwakilishwa na mabondia kama, Thomas Mashali, Mchumiatumbo, Francis Miyeyusho, Majia, Kanda Kabongo, na wengine wengi. Picha zote na www.sufianimafoto.com
 Wadhamini wa timu ya Taswa, Kampuni ya TSN, pia walikuwepo viwanjani hapo wakionyesha kinywaji cha Chilly Willy, kinachotengezwa na kampuni hiyo. Pichani ni baadhi ya warembo wanaotangaza bidhaa za kampuni hiyo, wakiwa katika meza yao.
 Beki wa Taswa Fc, Juma Ramadhan, (nyuma) akimdhibiti mshambuliaji wa Full Mabondia, wakati wa mchezo huo.
 Beki wa Taswa Fc, Muhidin Sufiani 'Sufianimafoto' (kulia) akimfinya mchezaji wa Full Mabondia, wakati wa mchezo huo jana.
 Beki wa Taswa Fc, Elius Kambili, akiambaa na mpira.
 Beki wa Taswa Fc, Salim (kulia) akiondosha moja ya hatari mbele ya Bondia, Mchumiatumbo.
 Kipa wa Full Mabondia, akiwa golini huku akiwa peku peku, wakati wa mtanange huo jana.
 Zahoro Milanzi wa Taswa Fc, (kushoto) akiambaa na mpira wakati wa mtanange huo.
 Wachezaji wa Taswa Fc, wakipasha kabla ya kuanza kwa mtanange huo jana.
Sufianimafoto (katikati) akipozi na Bondia Francis Miyeyusho (kushoto) na 'Chuji' (kulia) kabla ya kuanza kwa mtanange huo jana.
Benchi la Taswa Fc.
Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila 'Super D' akitoa maelekezo kuhuzu mchezo huo walipocheza timu ya mpira ya mabondia na TASWA FC picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com



Bonia Daudi Muhuzi akishindana na Mbuyu wa timu ya TASWA FC Majuto Omari wakati wa mpambano wao

Kocha wa kimataifa wa Mchezo wa Masumbwi Nchini Rajabu Mhamila ' Super D' akisisitiza jambo wakati wa mapumziko picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Mchezaji wa timu ya Taswa akipambana na bondia kuwania mpira


SUPER D BOXING COACH AKISISITIZA JAMBO WAKATI WA MAPUMZIKO WA MCHEZO HUO
Posted by MROKI On Monday, May 20, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo