
“Hii siyo mara yetu ya kwanza kuwapeleka warembo wetu mbugani. Tumekuwa tukifanya kila mwaka,” alisema Kalinga.
Kapinga alisema kuwa ziara hiyo imedhaminiwa na CXC Africa.
Shindano
la kumsaka Miss Tabata litafanyika Mei 31 katika ukumbi wa Da’ West
Park, Tabata.
Wadhamini wa shindano hilo ni Nipashe, Redds, Dodoma Wine, Nipashe,
Vayle Springs, Multichoice, Fredito Entertainment, CXC Africa, Brake
Point, Michuzi Blog na Saluti5.
Warembo
watakaoshiriki kwenye shindano hilo (pichani) linaloandaliwa na Bob
Entertainment na Keen Arts ni Madgalena Bhoke (21), Kabula Juma Kibogoti
(20), Upendo Dickson Lema (22), Hidaya David Mwenda (22), Aneth
Ndumbalo (19), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Musa
Kitereja (19), Rehema Kihinja (20), Pasilida Mandali (21), Brath
Chambia (23), Joaniter Kabunga (21), Recho Mushi (20),Caroline Sadiki
(20) na Suzan Daniel (18).
Warembo watano watachaguliwa kushiriki mashindano ya Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania.
Anayeshikilia taji la Miss Tabata kwa sasa ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.
0 comments:
Post a Comment