Miss Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred (kulia) akizungumza na Warembo wanaotarajia kuwania Taji la Redd's Miss Sinza 2013, wakati alipowatembelea katika Kambi yao ya mazoezi jana katika Ukumbi wa Meeda Sinza na kuwafunda kuhusu mashindano hayo kuelekea shindano hilo linalotarajia kufanyika Juni 7,mwaka huu kwenye Ukumbi huo. Katika shindano hilo Viingilio vitakuwa ni Sh. 20,000 kwa VIP na viti vya kawaida ni Sh. 10,000.
Shindano hilo limedhaminiwa na Mtandao wa www.sufianimafoto.com, kinywaji cha Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Clouds Media Group, CXC Africa, Saluti5 na Fredito Entertainment.
Shindano hilo limedhaminiwa na Mtandao wa www.sufianimafoto.com, kinywaji cha Dodoma Wine, Chilly Willy Energy Drink, Clouds Media Group, CXC Africa, Saluti5 na Fredito Entertainment.
Miss Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred (katikati) akipozi na warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Sinza 2013, wakati alipowatembelea kwenye Kambi yao ya mazoezi katika Ukumbi wa Meeda Sinza.
Miss Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred (katikati) akipozi na warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Sinza 2013, wakati alipowatembelea kwenye Kambi yao ya mazoezi katika Ukumbi wa Meeda Sinza. Picha zote na www.sufianimafoto.com.
***********
Na Mwandishi wetu
Redds Miss Tanzania
2012 ambaye pia ni Redds Miss Sinza, Brigitte Alfred amewataka warembo
wanaowania taji la mwaka huu la kituo cha Sinza kutomuangusha kwa
kufauata nyayo zake katika shindano lililopangwa kufanyika Juni 8 kwenye
ukumbi wa Meeda Club.
Brigitte alisema hayo
juzi alipotembelea warembo wanaowania taji la mwaka huu katika
kinyang’anyiro hicho kilichodhaminiwa na bia ya Redds Origional, Dodoma
Wine, Clouds Media Group, Chilly Willy Energy Drink, Fredito
Entertainment, CXC Africa, Saluti5.com na Sufiani Mafoto blog.
Alisema kuwa warembo
wa kituo hicho wanakazi kubwa ya kushinda taji hilo na baadaye Miss
Kinondoni na Miss Tanzania kama yeye alivyofanya.
Alifafanua kuwa siri
kubwa ya mafanikio ni kujituma na kuwa na nidhamu ya hali ya juu kwani
hata yeye alifundishwa na matroni wa sasa, Mwajabu Juma na waandaaji ni
wale wale.
“Sioni sababu ya
kushindwa kufanya vyema katika mashindano haya, Redds Miss Sinza ndiyo
inatetea taji la Miss Kinondoni na Miss Tanzania pia, hivyo macho ya
wadau wote wa urembo yatakuwa kwenu na ndicho kitongoji kinachofunga
mashindano ya ngazi ya chini, mnatakiwa kujituma na kuwafanya majaji
kuwa na kazi ya ziada kumpata mshindi,” alisema Brigitte.
Alisema kuwa wadau wa
masuala ya urembo wanaangalia Sinza mwaka huu itafanya nini baada ya
mafanikio makubwa ya mwaka jana. “Sisi tumejenga msingi mkubwa na
kuleta heshima kwa wakazi wa Sinza, Kinondoni na Tanzania kwa ujumla,
nanyi mna jukumu hilo,” alisema.
Mratibu wa mashindano
hayo, Majuto Omary alisema kuwa maandalizi yamekwisha kamilika na
kiingilio ni sh 10,000 kwa viti vya kawaida na shs 20,000 kwa viti vya
VIP. Alisema kuwa wanakamilisha maandalizi ya burudani ya siku hiyo
ambayo itakuwa ya aina yake.
0 comments:
Post a Comment