Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na baba wa mtoto, Elizabeth Nora kutoka Dodoma aliyelazwa
katika Hospitali ya CCBRT, wakati Makamu alipofika hospitalini hapo leo
Mei 23, 2013 kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya
Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisikiliza maelezo kutoka kwa Dokta wa Hospitali ya CCBRT, wakati
alipokuwa akitembelea katika wodi za wagonjwa waliolazwa katika
Hospitali hiyo, alipofika hospitalini hapo leo, kwa ajili ya kushiriki
katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa
Fistula. Kulia ni Mtoto Boniface Patrick akiwa na Baba yake, Patrick
Luwao, Wakazi wa Dodoma, akiwa amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji na
kuongezewa sehemu ya mguu uliokuwa mfupi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Stellah Nzyemba, ambaye awali alikuwa mgonjwa na baada
ya kutibiwa katika Hospitali hiyo ya CCBRT na kupona ameajiriwa ili
kuwasaidia wagonjwa wa Fistula. Makamu alifika hospitalini hapo leo kwa
ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya
Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akitembelea katika Wodi ya wagonjwa wa Fistula, wakati Makamu alipofika
hospitalini hapo leo kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku
ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula.
Makamu wa Rais Dkt Bilal, akimjulia hali mtoto mgonjwa aliyelazwa katika Hospitali hiyo ya CCBRT
Baadhi
ya wasichana waliokuwa wakiugua ugonjwa huo na kutibiwa katika Hospitali
ya CCBRT, ambao kwa sasa wanapewa mafunzo ya kufanya kazi za mikono.
0 comments:
Post a Comment