MAANDALIZI ya Redds Miss Moshi 2013 yatakayofanyika Jumamosi, May 18 katika ukumbi wa Aventure, Mjini hapa yameanza kushika kasi.
Akizungumza na Tanzania Daima, mratibu wa mashindano hayo, Mkurugenzi
wa kampuni ya New Vision plan inayohusika na kazi za kuandaa mashindano ya ulimbwende, Moses Komba alisema kuwa jumla ya walibwende wapatao kumi19 watachuana kumsaka malkia wa Moshi.
Moses alisema tayari mchujo wa kwanza umeshafanyika ambapo warembo wote wameshaingia kambini kujifua na kuongeza kwamba mashindano ya mwaka ambayo ni ya pili tangu yaanzishwe yatakuwa ni ya aina yake.
“Maandalizi yameshaanza, warembo wote wapo kambini hapa katika ukumbi wa aventure, kila kitu kinakwenda sawana tunategemea kushuhudia kitu tofauti nay ale ya mwaka jana,” alisema Komba.
Kuhusu swala la udhamini alisema bado hilo ni tatizo huku wadhamini wakuu Redds na kampuni ya panone kwa kujitolea kudhamini mashindano hayo.
Akitangaza viingilio katika mashindano ya mwaka huu, Komba alisema kuwa kwa viti vya dhahabu viingilio vitakuwa sh. 50,000, viti vya V.I.P vitakuwa ni sh. 30,000 na viingilio vya kawaida ni sh. 15,000.
Kwa upande baadhi ya washiriki wa Redds Miss Moshi, wakizungumza na Gazeti hili katika kambi ya mazoezi, Jacky Mushi, Winlady Mushi, Aichi Edwin na Rayness White walisema kuwa wabnatarajia kutumia uzoefu watakaoupata kutoka katika mashindano hayo kulitumikia jamii hasa wale waishio katika mazingira magumu.
Mashindano ya Redds Miss Moshi 2013 yatakayofanyika katika ukumbi wa
Aventure, yanadhaminiwa na Redds, Panone na Baba G na Zoom Net Printers ambapo kwa upande wa burudani alisema atakuwepo msanii
mkongwe wa kizazi kipya Dully Sykes akisindikizwa na wasanii wengine
kutoka Moshi.
0 comments:
Post a Comment