Meneja Masoko wa kinywaji cha Chilly Willy kinacho sambazwa na kampuni ya TSN Group, Yohana Manoli (Kushoto)
akimkabidhi jezi mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary (wa kwanza kulia)
katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye mgahawa wa
Hadees. Kulia ni Meneja Uhusiano wa TSN Group, Meshack Nzowah.
*****************
Kinywaji maarufu cha kuongeza nguvu, Chilly Willy Energy Drink kimetoa msaada wa jezi na
mipira kwa timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa
FC na timu ya Netiboli, Taswa Queens kwa ajili ya kutumika michezo yake
mbali mbali.
Meneja
Masoko wa Kampuni ya TSN Group kinachosambaza kinywaji cha Chilly Willy
Yohana Manoli alikabidhi vifaa hivyo kwa mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto
Omary katika hafla fupi iliyopfanyika kwenye mgahawa wa Hadees uliopo
katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Manoli
alisema kuwa sababu kubwa ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Taswa SC ni
kutambua mchango wa waandishi wa habari katika kuendeleza michezo nchini
na hasa ukizingatia kuwa kinywaji cha Chilly Willy hakina kilevi na ni
maalum kwa wanamichezo.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TSN
Group, Meshack Nzowah alisema kuwa kinywaji chao cha Chilly Willy kina
ubora wa kimataifa na wanaamini kuwa wanamichezo na wanajamii wataanza
kutumia kinywaji hicho katika shughuli mbalimbali.
“Chilly
Willy ni kinywaji ambacho hakina kilevi, kina ubora wa kimataifa na
kutokana na hilo, kampuni ya TSN Group ikaamua kukisambaza nchini kwa
lengo la kutoa bidhaa iliyobora zaidi, tunaamini wanamichezo wataanza
kutumia hiki na vile vile ni maalum kwa waandishi wa habari na wadau
wengine nchini,” alisema Nzowah.
Mwenyekiti
wa Taswa SC, Majuto Omary aliipongeza kampuni inayosambaza kinywaji cha
Chilly Willy na kuwaomba waandishi wa habari kuanza kutumia kinywaji
hicho. Majuto alisema kuwa Chilly Willy imetambua mchango wa Taswa SC katika kuendeleza michezo na kutoa msaada huo.
“Ni
faraja kubwa kuwa na kinywaji hiki hapa nchini na hasa kwa kutujali
wana habari, kwa vifaa hivi, Taswa FC na Taswa Queens zitakuwa na nguvu
na ubora kama wa Chilly Willy,” alisema Majuto.
Majuto
alisema kuwa jezi hizo watazizindua rasmi Jumapili katika mechi dhidi
ya timu ya kombaini ya mabondia wa ngumi za kulipwa nchini itakayochezwa
kwenye uwanja wa Leaders Club kuanzania saa 5.00 asubuhi.
Alisema
kuwa timu ya mabondia itaongozwa na bondia mkongwe nchini, Rashid
“Snake Man” Matumla na mabondia wakali wengine kama Francis “SMG” Cheka,
Cosmass Cheka, Mbwana Matumla, Karama Nyilawila, Maliki
Kinyogoli, Hassan Matumla, Daudi Mhunzi, Saidi Yazidu, Francis Miyeyusho
, Thomas Mashali, Charles Mashali na wengine wengi.
0 comments:
Post a Comment