Nafasi Ya Matangazo

May 07, 2013

Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu Wiki ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii itakayofanyika mjini Dodoma kuanzia Mei 13-18. Kushoto ni Mkuu wa Mahusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde na Mkaguzi Mkuu wa Ndani SSRA, Peter Mbelwa.
 Mkuu wa Mahusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde akizungumza  wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu Wiki ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii itakayofanyika mjini Dodoma kuanzia Mei 13-18. na Mkaguzi Mkuu wa Ndani SSRA. Kulia ni Mkurugenzi  Mkuu wa Mamlaka Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka na Mkaguzi Mkuu wa Ndani SSRA, Peter Mbelwa. 
Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), imeandaa Maonyesho ya Wiki ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, ambayo yanatarajiwa kufanyika Mei 13 hadi 18 mjini Dodoma.

Akizungumza na Habari Mseto, Mkurugenzi wa SSRA, Irene Isaka, alisema, makampuni na mashirika mbalimbali yanatarajia kushiriki wiki, ambayo mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Kikwete.

Alisema kuwa, maonyesho hayo itakuwa ni pamoja na mifuko shiriki kutoa elimu kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla, juu ya huduma ambazo zinapatikana na tija yake katika taifa.

Aidha, Irene aliongeza kuwa, SSRA inawataka wanachama wa PSPF kuondoa hofu juu kutokuwepo kwa mafao yao katika mfuko huo, na kwamba mafao yao yako salama na hakuna kitakachopoteza mafao ya wanachama hao.

Alisema kuwa, mfuko wa PSPF utakuwa ukipewa bilioni 50 kila mwaka kwa ajili ya kwa ajili kuendelea kufanya kazi zake kama kawaida .

Irene pia, aliwataka wanachama wa mifuko mbalimbali kuwasilisha michango yao kwa wakati ili kuweza kutatua changamoto zilizopo katika mifuko kutokana na SSRA kutoa miongozo juu ya uendeshaji wa mifuko hiyo.

Alibainisha kuwa, mifuko yote imepewa miongozo katika uendelezaji huduma wanazozitoa ikiwamo ya mafao kwa wafanyakazi wanaostaafu.

Alisema kuwa tatizo lililokuwepo kwa mifuko ya PPF na NSSF, kujitoa kwa wingi kwa wanachama wake, jambo linalochangiwa na waajiri, hali ambayo SSRA inataka kuwafuatilia waajiri wanaowanyima wafanyakazi haki zao.


Posted by MROKI On Tuesday, May 07, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo