Mei mosi, jumatano iliyopita kupitia televisheni
za ITV na Clouds TV katika kipindi cha 7 cha GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE tuliona timu ya Tanzania,Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad
ikifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali pamoja na timu ya Kenya, Kenneth
Kumau na Wills Ogutu, kutoka Nairobi ambao ndio walizishinda timu zote katika
sehemu hii ya saba.
Wakenya walifanikiwa kupita
katika hatua zote lakini wakapata ushindani kutoka kwa Waghana katika hatua ya
Bullyese. Ilikuwa ni hatua ngumu lakini Wakenya ndio waliofanikiwa kufikia
hatua ya pesa ukutani ambapo walifanikiwa kujishindia dola za kimarekani 1,500.
Daniel, Mwalimu, Kenneth na
Wills wataendelea kuziwakilisha nchi zao kuwania kitita cha dola za kimarekani
250,000 na nafasi ya kuvishwa taji la ubingwa wa Pan-African. Timu hizi mbili zitatakiwa
kujiandaa vizuri zaidi na kujiamini ili ziweze kujinyakulia ushindi.
Meneja wa kinywaji cha Guinness,Devis
Kambi alisema, “Hongera kwa Daniel na Mwalimu kwa kufanikiwa kufuzu kuingia
nusu fainali. Bado tunaendelea kuburudika na mashindano ya GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE baada ya kuona robo fainali wiki iliyopita. Sasa ushindani utakuwa
mkali zaidi kwa kuwa tumebakiwa na timu nane tu katika nusu fainali. Timu zote
sasa zinahitaji maandalizi ya kutosha ili ziweze kufanya vizuri katika hatua hizi
za mwisho za kuelekea fainali. Kila la heri kwa timu zinazofuata kucheza wiki
hii!”
Timu zitakazo shiriki katika
robo fainali ya tatu ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE :
Kutoka Kenya watakuwa ni
Enpantus Nyambura(24) na Samuel Papa(23) kutoka Nairobi, watavaa jezi nyekundu.
Wakitarajia kufanya vyema zaidi kuliko awali Enphatus atakuwa kichwa cha timu
wakati Samuel ataonesha kipaji chake cha kusakata kabumbu.
Watakaovaa jezi za bluu
watakuwa ni wanafunzi wa Ghana, George Duah (21) na Yahya Issaka(20) kutoka
Takoradi. George ni kichwa cha timu wakati Yahya ndiye atakayechezea
mpira.Walifanikiwa kufuzu kuingia katika fainali ya kitaifa baada ya
kujishindia dola 3,000.
Kutoka Cameroon Florent
Tonya(29) na Christian Lolo Mboko(24) kutoka Douala watavaa jezi za kijani
katika robo fainali ijayo na katika hatua ya kitaifa wajishindia dola 3,000. Florent
atajibu maswali wakati Christian atakuwa akionyesha kipaji chake cha kucheza
soka.
Ghana itawakilishwa na
Jonathan Naab(25) kutoka Tindogo na Desmond Odaano(26) kutoka Larteh watavaa
jezi nyeusi katika robo fainali ijayo. Awali timu hii ilijishindia dola za
kimarekani 5,500 katika hatua ya kitaifa. Jonathan atakuwa akipima maarifa yake
wakati Desmond ataichezea mpira.
Robo fainali ya tatu ya
Pan-African itarushwa katika televisheni za ITV na Clouds TV usikose kushuhudia
timu kutoka Afrika Mashariki ikipambana vikali na nchi zingine za Afrika.
Wapenzi wa kipindi hiki cha
Guiness football challenge barani Afrika wanakumbushwa kwamba wanaweza kushiriki
kwa kufuatilia kwa karibu. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com kwa kupitia simu ya mkononi.
Hakikisha kuufwatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE kwa habari mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania
GUINNESS
FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni
ya kimataifa ya Endemol. Usikose
kuangalia na kufuatialia kipindi hiki katika runinga yako kupitia televisheni
za ITV na Clouds TV kila siku ya Jumatano usiku saa 3:15 ITV na saa 2:15 Clouds
TV.
Usisahau
kuwa na chupa ya bia uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki.
Tafadhali kunywa kistaarabu-
Hairuhusiwi kuuzwa kwa wale wenye umri chini ya miaka 18.
0 comments:
Post a Comment