Hotuba ya
Kambi ya Upinzani Bungeni kwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
iliyokuwa ikisomwa na Msemaji (Waziri Kivuli wa Wizara hiyo) ambaye pia ni
Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema) Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Bungeni imesimamishwa
kwa kile kilechoelezwa kukiuka taratibu za Bunge.
Akisimama
kuomba Muongozo wa Spika, Mbunge wa CCM jimbo la Mbozi Mashariki, Godfrey
Weston Zambi, aliliambia Bunge kuwa Hotuba hiyo katika kurasa zake 12 za awali
imejaa maneno ya uchochezi kwa Serikali ya CCM.
Zambi
alisema miongoni mwa maneno hayo ya Uchochezi ni yale ya kusema kuwa Serikali
ya CCM kuwashambulia wanahabari kwa kuwapiga, kuwang’oa kucha, kuwamwagia tindi
kali na kuwaua jambo ambalo sio kweli.
Kufuatia
hatua hiyo Spika wa Bunge Anne Makinda alipokea Mwongozo huo na kuliahirisha
Bunge hadi Hotuba hiyo itakapo pitiwa upya ndipo iletwe tena Bunge hapo.
0 comments:
Post a Comment