Kesho
jumamosi wabunge tumealikwa kwenye semina kuhusu sera ya Gesi Asilia.
Tumegawiwa tayari nakala zetu, tena zipo kwenye lugha ya kimombo.
Ikumbukwe
kwamba kuanzia tarehe 22 - 23 Mei 2013 kutakuwa na mjadala wa bajeti ya
Wizara ya Nishati na Madini. Semina hii ni maandalizi ya Bajeti hii.
Jambo
la kushangaza ni kwamba wakati sera ya Gesi Asilia ipo kwenye rasimu na
ndio kwanza wabunge tumeletewa kutoa maoni, Serikali tayari imetangaza
tena kugawa vitalu vya Mafuta na Gesi kwenye Bahari kuu na Ziwa
Tanganyika Kaskazini.
Zabuni
hii mpya ya vitalu vya utafutaji imetolewa wakati kuna maamuzi ya Bunge
kuzuia ugawaji huu mpya mpaka sera ya Gesi Asilia na Sheria ya Gesi
vikamilike.
Haraka
hii ya serikali kugawa vitalu bila sera wala Sheria inatoka wapi?
Nitashangaa sana wabunge kukimbilia posho za semina hii na kuhalalisha
maamuzi yasiyo zingatia maslahi ya Taifa Kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Uamuzi wa kugawa vitalu vipya bila kwanza kuwepo Kwa sera na Sheria
mpya unapaswa kupingwa Kwa Nguvu zote.
Tafuta mbunge wako, mwambie asikubali maamuzi haya ya serikali.
Tumalize kwanza sera na Sheria ndio tugawe vitalu vipya. Gesi sio viazi, haiozi.
ZITTO KABWE-MB.
ZITTO KABWE-MB.
0 comments:
Post a Comment