Robo
fainali ya kwanza ya Pan-African GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ ilifanyika jana
usiku ambapo mashabiki wa Afrika masharik i walikuwa wakishangilia timu za nchi
zao. Washiriki mahiri kutoka Cameroon,Ghana,Kenya ,Uganda na Tanzania
walikutana uso kwa uso ili kushindania dola za kimarekani 250,000 na kutwaa ubigwa wa Pan-African.
Timu
ya Afrika mashariki iliyoweza kufuzu kuingia nusu fainali kutoka kipindi cha kwanza
ni Francis Ngigi na Kepha Kimani kutoka Kenya. Japokuwa hawakufanikiwa kufikia
hatua ya mwisho ya ukuta wa pesa wa GUINNESS lakini walifanikiwa kuingia nusu
fainali. Emerand Tchouta(24) na Abdul Salam(25) kutoka Cameroon walionesha kuwa
wao ni wachezaji wazuri ambapo walifanikiwa kufikia hatua ya mwisho ya ukuta wa
pesa. Katika hatua ya mwisho, ambapo walifanikiwa kujipatia dola za kimarekani 5,000
kuongezea walizokuwa nazo waliposhinda mwanzoni dola 1,500.
Timu
zitahitaji kuwa na umoja na kujiamini ili kuweza kujiandaa kwa hatua
zinazofuata. Timu moja kutoka Dar es Salaam Tanzania wataingia uwanjani wiki
ijayo itakua na Daniel Msekwa(21) na Mwalimu Akida Hamad(26).
Meneja
wa kinywaji cha Guinness, Davis Kambi alisema, “Robo fainali ya GUINNESS FOOTBALL
CHALLENGE ilisisimua katika runinga ambapo Francis na Kepha walifanikiwa
kuiwakilisha Afrika mashariki katika nusu fainali. Timu kutoka Kenya na
Cameroon zimefuzu kuingia nusu fainali, wiki
ijayo washiriki wengine watakutana ili kujua ni nani atashinda na kufuzu hatua
ya nusu fainali. Nawatakia wote kila la heri”.
Timu
nne zitakazo shiriki wiki ijayo kutafuta nafasi ya kuingia nafasi ya nusu
fainali ni:
Watakao
kuwa na jezi za bluu ni Daniel Msekwa (21) ambaye ni kichwa cha timu, na
mwenzie Mwalimu Akida Hamad (26). Walifanikiwa kujishindia dola za kimarekani 5,500 katika mashindano ya
Afrika Mashariki hivyo wana nafasi kubwa ya kufuzu nusu fainali.
Wenye
jezi nyekundu watakuwa wakenya, kocha wa vijana Kenneth Kamau(23) na dereva
Wills Ogutu (30) wote kutoka Nairobi. Ingawawa hawakufanya vizuri sana katika
sehemu zilizopita lakini wanaweza kufanya vizuri wiki ijayo wakijipanga vizuri.
Archille
Stephanie na Martial Toubou kutoka Douala Cameroon watavaa jezi za kijani. Archille
atajibu maswali wakati Martial ataonesha uwezo wake wa kucheza soka.
Walifanikiwa
kujishindaia dola 4,000 katika sehemu zilizopita.
Jezi nyeusi watakuwa ni Dennis Nyaku(25) na
Francis Nyarko(27) wote kutoka Ho Ghana
ambapo walifanikiwa kujishindia dola 1,500 katika mashindano ya kitaifa. Dennis
atakuwa kichwa wakati Francis atakuwa akionesha
uwezo wake wa kusakata kabumbu na kuweka chini vifaa vya uchoraji.
Wapenzi
wa kipindi hiki cha Guiness football challenge barani Afrika wanakumbushwa
kwamba nao wanaweza kushiriki kwa kufuatilia kwa karibu. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika tovuti ya m.guinnessvip.com kwa kupitia simu yako ya
mkononi.
Robo fainali ya pili ya
Pan-African itaoneshwa katika televisheni za ITV na Clouds TV kila jumatano saa
3:15 ITV na Clouds TV saa 2:15 usiku.
Hakikisha kuufwatilia ukurasa
wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali-www.facebook.com/guinnesstanzania
GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha
mchezo wa soka kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol. Usikose kuangalia na kufuatialia kipindi hiki
katika runinga yako kupitia televisheni za ITV na Clouds TV kila siku ya
Jumatano usiku.
Usisahau kuwa na chupa ya bia uipendayo ya Guiness wakati unaangalia kipindi hiki.
Tafadhali
kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa wale wenye umri chini ya miaka 18.
0 comments:
Post a Comment