Na Mwandishi wetu
Wakati timu ya netiboli ya waandishi wa habari za michezo
nchini, Taswa Queens imeishushia kisago cha mabao 36-2 timu ya kombaini wa
walimu wa Wilaya ya Kibiti, wenzao wanaume, Taswa FC imechapwa mabao 2-0 na
timu ya kombaini ya Walimu kwa upande wa mpira wa miguu.
Huu ni ushindi wa pili kwa Taswa queens tokea kuanzishwa
kwake April 6 mwaka huu na kuifunga timu ya Kiliflora queens kutoka mkoani
Arusha kwa mabao 28-8 katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa TCC,
Chang’ombe.
Ikicheza kwa uelewano mkubwa, Taswa Queens iliwabana
wapinzani wao kila kona na kufunga mabao 18-1 hadi mapumziko. Katika mchezo huo
Imani Makongoro kutoka Mwananchi Communications Limited aliyechezea nafasi ya
GA alifunga mabao 16 na Amina Mussa wa BTL aliyechezea mafasi ya GS alifunga
mabao 20.
Wachezaji wengine waliocheza mechi hiyo ni Clensenia
Tryphone (Tanzania Daima), Elizabeth
Mbassa, Sharifa Mustapha na Johari William wote wa Business Times Limited (BTL).
Kwa upande wa soka, mabao yaliyofungwa ndani ya dakika
10 na timu ya kombaini ya walimu,
yalidumu muda wote wa mchezo na kuifanya timu hiyo kutoka uwanjani kichwa
chini. Mabao ya walimu yalifungwa na Hamidu Mwichande na Juma Kimondoo.
Walimu walionyesha uwezo mkubwa katika dakika 25 za mwanzo
na kuifanya Taswa FC kutweta katika muda huo, hata hivyo kibao kilibadilika na
Taswa FC kutawla muda uliobaki huku ikosa nafasi kadhaa za wazi.
Kutokana na kipigo hicho, Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto
Omary alisema kuwa wanajipanga kulipiza kisasi kwa kurejea tena kucheza Kibiti.
“Tumefungwa kutokana na uchovu sa safari, tulifika saa 9.15 alasiri, tukapata
chakula na kwenda moja kwa moja uwanjani, hatukuwa wanyumbulifu, hata hivyo
tunaahidi kurejea tena nakulipiza kisasi,” alisema Majuto.
Kiongozi wa timu ya walimu, Hamza Malwile, alisema kuwa
wamefuraishwa na ujio ya waandishi na kutoa hamasa kubwa ya michezo. Malwile
ambaye ni mwenyekiti wa timu, alisema kuwa watajipanga kwa ajili ya mechi ya
marudiano.
0 comments:
Post a Comment