Nafasi Ya Matangazo

April 16, 2013

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwaasa Waheshimiwa Wabunge kutumia Lugha ya Kistaarabu kuchangia mijadala Bungeni.
 
Spika wa Bunge Anne Makinda awaasa Wabunge kutumia Lugha ya Staha ambayo ni ya Kibunge wakati wa kuchangia mijadala Bungeni. Mhe. Makinda amesema, kuendelea kutumia lugha ya matusi, kejeli na maudhi kwa baadhi ya Waheshimiwa Wabunge ni kuendelea kuliondolea hadhi Bunge. 

Pamoja na hilo, wabunge wanatakiwa kujikita katika kuchangia hoja zenye kutataua matatizo ya wananchi ili kutimiza wajibu wa kila mbunge wa kuwa wakilisha wananchi. Mhe. Makinda , amesema, fursa ya kila Mbunge kuchangia lazima ilenge kutatua matatizo ya wananchi na sio kutukanana na kusahahu jukumu lilomblele ya kila Mbunge. 

Katika Picha ni baadhi ya waheshimiwa Wabunge waliochangia mjadala wa kupitisha Makadirio na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2013/14 Bungeni Mjini Dodoma leo.
Mbunge wa Mwibara Mhe. Kangi Lugola, akiomba Mwongozo kwa Spika Bungeni
Mhe. Catherine Magige, Mbunge wa Viti Maalum (CCM) akichangia Mjadala leo
Mbunge wa Temeke Mhe. Abbas Mtembu akichangia Mjadala
Mbunge wa Ukerewe Mhe. Salvatory Machemli akichangia Mjadala Bungeni leo
 Mbunge wa Viti Maalum (CUF) Mhe. Kuruthum Mchuchuli akichangia  kwa hisia mjadala leo Bungeni.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na teknolojia Mhe. January Makamba akijibu baadhi ya hoja zilizochangiwa Bungeni leo.Picha zote na Owend David wa Bunge
Posted by MROKI On Tuesday, April 16, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo