Timu ya Mbezi inayohusisha waendasha pikipiki
maarufu kama bodaboda ikishangilia ushindi mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza
wa michuano ya Mpinga Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay
police. Mbezi iliifunga makondeko mabao 7-6 na kuibuka washindi
Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Pereira Silima akikabithi mfano wa hundi ya shilingi
millioni moja kwa captain wa timu ya Mbezi Ally Shila Kulola baada ya
timu yake kuibuka washindi wakwanza wa michuano ya mpinga Cup kwa kushinda
Makondeko mabao 7-6
Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde akikabithi
zawadi kwa captain wa timu ya makondeko Stanley Peter mara baada ya kuibuka
washindi wa pili wa mashindanoo ya mpinga Cup yaliyohusisha waendasha pikipiki
(bodaboda) kwa muda wa wiki moja katika viwanja vya oyesterbay polisi.
Kushoto pembeni ni kiongozi wa timu ya makondeko bwana Mneke S Mneke
Michuano ya mpinga Cup imemalizika rasmi jana
baada ya mchezo wa fainali thidi ya timu ya Mbezi na makondeko ambapo,
timu hizo zilitoka sare ya bao 2 -2 na kuingia kwenye mkwaju wa penalti
ambapo timu ya kawe iliibuka na ushindi wa mabao 7 -6 .
Katika michuano hiyo iliyodumu kwa muda wa wiki
nzima na kushirikisha timu nane kutoka katika mkoa wa kipolisi wa kinondoni
timu ya mikocheni Iliibuka kuwa mshindi wa tatu wa michuano hiyo.
Akiongea wakati wa kufunga michuano hiyo mgeni
rasmi Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Pereira
Silima alisema” tunawashukuru waandalizi wa michuano hii na wadhamini
ambao ni Airtel, Mr price, home shoping center na Rotary Club Dar es Saalam kwa
ushirikiano wao mkubwa na mchangao wao katika kuhakikiksha mashindano haya
yanafanyika kwa mafanikio.
Hii nijitahada ya pekee kuunganisha michezo na
elimu ya usalama barabarani. Tumegundua vipaji vingi hapa tunawaasa wachezaji
hawa wajiendeleze mbali na kuendesha pikipiki kwa muda wa ziada wataweza
kucheza mpira na kupata njia nyingine ya kipato kwa michezo ni ajira.
Naye Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani
SACP. Mohamed Mpinga amewashukuru washiriki wote wa michuano hii na kusisitiza
wananchi na watanzania kwa ujumla kutii sheria bila shurutishi.
Akiongea kwa niaba ya wadhamini Afisa Uhusiano
wa Airtel Jane Matinde alisema” mashindano haya yamekuwa ya mvuto mkubwa kwa
washiriki na wadau wa michezo zaidi tumeshuhudia jinsi mafunzo ya elimu ya
usalama barabarani yalivyoendesha na kuelimisha watumiaji wa barabara waliokuwa
wakihudhuria hapa.
Tunaamini kuendelea na juhudi hizi
tutaweza kupunguza idadi za ajali barabarani. Airtel tunaahidi kuendelea
kushirikiana na jeshi la polisi usalama barabarani katika shughuli
mbalimbali za uelimishaji umma juu ya sheria za barabarani
Michuano ya mpinga cup kwa wilaya ya kinondoni
imefika tamati hapo jana na mpango ni kuwa na michuano hii pia katika mkoa wa
ilala na temeke na kisha kuendelea na michuano hii nchini nzima.
0 comments:
Post a Comment