Wakalawa Miss Tanzania 2012 kutoka Mkoa wa Shinyanga, Asela Magaka
akichangia madawakati wa semina ya siku mbili ya Mawakala wa Redds Miss
Tanzania 2012.
*****
Na Mwandishi Wetu
MAWAKALA wote walioteuliwa kuandaa mashindano ya
urembo nchini mwaka huu "Redd's Miss Tanzania" leo wanatarajiwa
kushiriki katika semina maalumu itakayofanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi kwenye
hoteli ya Girraffe iliyoko jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana jijini, Mkurugenzi wa kampuni ya Lino Agency, Hashim Lundenga, alisema kuwa mawakala watakaoshiriki semina hiyo ni wa kuanzia ngazi ya kanda, mikoa na vitongoji vyote vya mkoa wa Dar es Salaam.
Lundenga alisema kuwa maandalizi ya semina hiyo yamekamilika na mawakala kutoka mikoani walianza kuwasili jijini tangu jana asubuhi na katika mialiko waliyotumiwa wamesisitizwa kufika bila kukosa ili kupata maelekezo kabla ya kuanza kuandaa mashindano yao ya ngazi husika.
Alisema kuwa kila mwaka kamati yake hutoa maelekezo kulingana na kanuni na taratibu zilizopitishwa na kamati hiyo na vile vile kuwapa mwangaza mawakala ni makampuni na taasisi zipi wanazoruhusiwa kuomba udhamini ili wasiende tofauti na mdhamini mkuu wa shindano hilo ngazi ya taifa ambao ni kampuni ya bia nchini TBL kupia kinywaji chake cha Redd's original.
"Tunaamini semina itafanyika kama ilivyokusudiwa na mawakala watapewa mbinu za kukabiliana na changamoto katika kutekeleza majukumu yao," alisema Lundenga.
Mrembo kutoka katika kitongoji cha Sinza, kanda ya Kinondoni, jijini, Brigitte Alfred, ndiye mrembo anayeshikilia taji hilo la taifa aliyelitwaa kutoka kwa Salha Israel wa Ilala.
Hata hivyo Brigitte ndiye atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya dunia mwaka huu na mrembo atakayeshinda taji hilo baadaye mwaka huu atashiriki fainali hizo za dunia mwakani.
0 comments:
Post a Comment