KUONGEZEKA
kwa joto katika Pwani ya Tanzania , kupotea kwa baadhi ya viumbe katika bahari ya
hindi na kumezwa kwa visiwa kumeelezwa kuwa ni miongoni mwa athari zitokanazo
mabadiliko ya tabia nchi.
Hayo
yameelezwa leo na Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia
Ngosi Mwihava katika warsha ya wadau ya programu ya kitaifa ya kuhimili athari
zitokanazo na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi katika ukanda wa pwani
inayoendelea mjini Bagamoyo.
Injinia
Mwihava ameeleza kuwa, athari nyingine zitokanazo na madhara hayo ni pamoja navisiwa baridi
kuingiliwa na maji ya chumvi, vina vya bahari kuongezeka na kwa kuwa viumbe
katika bahari hupotea inaweza kupelekea uchumi wa wakazi wengi wa mwambao
kudidimia kwani hutegemea zaidi uvuvi.
Tanzania
kama nchi “Ina mkakati wa kuongeza uelewa kwa kushirikiana na wadau juu ya
dhana ya namna ya kukabiliana na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi
kwa kushirikiana na wadau na wananchi wa kawaida kwa kutumia sayansi na elimu
asilia ikiwa ni pamoja na kufuga samaki iliwaweze kusaidiaa kipindi ambacho
watakuwa wamepotea.
Kwa
upande wake mkurugenzi wa mradi wa pwani bwana Baraka kalangale ameeleza kuwa
ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi mradi wake unawajengea
uwezo wananchi katika eneo hilo kupitia
mafunzo na ushirikishwaji.
“Vijiji
vingi vimeathirika na masuala haya ya mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni pamoja
na kijiji cha mbuyuni katika wilaya ya pwani kwani kipo katika hatari ya
kumong’onyoka kabisa, alisisitiza.”
Warsha
hiyo inayohusisha wadau kutoka mashirika mbali mbali yanayojihusisha na masuala
ya mazingira na serikali kuu imefadhiliwa na shirika la misaada la watu wa
marekani (USAID)
0 comments:
Post a Comment