Nafasi Ya Matangazo

March 07, 2013


Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal leo amefungua Mkutano wa pili wa Mwaka wa wadau wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) jijini Dar es Salaam na kuzindua uuzwaji wa Nyumba za mradi wa Mfuko huo pamoja na Uchangiaji wa hiyari kwa Watu wasio watumishi wa Umma.

Pichani Meza kuu kutoka kushoto kwenda kulia ni Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, Katibu Mwenyekiti wa Bodi ya udhamini  PSPF, George Yambesi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu.

Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimkabidhi kitambulisho chake Mwalimu Winfrey Ibrahim Banda baada ya kujiunga na mfuko huo kupitia uchangiaji wa hiyari wakati wa Uzinduzi wake.

Sehemu ya wadau wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea ndani ya Mkutano huo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhan Dau (kushoto) akisalimiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema wakati viongozi hao wawili walipokutana katika Mkutano Mkuu wa wadau wa PSPF jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo wa PSPF, Adam Mayingu.

Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhan Dau (kushoto) akisalimiana Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa wakati viongozi hao wawili walipokutana katika Mkutano Mkuu wa wadau wa PSPF jijini Dar es Salaam leo. Kuliani ni Mwenyekiti wa Bodi ya udhamini  PSPF, George Yambesi


Wadau wa Mfuko wa PSPF walipokuwa wakijiandikisha muda mfupi kabla ya kuanza kwa mfuko huo.


Wasanii wa kundi la Ngoma za maonesho wakitoa burudani kwa wageni mbalimbali waliokuwa wakihudhuria mkutano huo.


Mzee Kassim Mapili akicharaza nyuzi za Gitaa lake chini ya Kundi zima la Mjomba Band wakati wa Ufunguzi wa Mkutano huo.


Mjomba, Mrisho Mpoto akighani mashairi yake na kumwaga sifa kede kede za Mfuko wa PSPF na manufaa yake kwa wadau na wanachama.


Sehemu ya wadau wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea ndani ya Mkutano huo jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Bodi ya udhamini  PSPF, George Yambesi akizungumza wakati wa Mkutano huo.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, akizungumza mbele ya wadau wa PSPF.



Sehemu ya wadau wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea ndani ya Mkutano huo jijini Dar es Salaam leo.
Posted by MROKI On Thursday, March 07, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo