MTOTO wa Rais wa kwanza wa Kenya, Marehemu Rais Jomo
Kenyatta, ambaye alikuwa anagombea Urais kwa tiketi ya Chama cha TNA, Uhuru
Kenyata ameshinda nafasi hiyo baada ya kumwangusha mpinzani wake Raila Odinga.
Hadi saa 8:35 usiku wa leo Uhuru alikuwa mbele kwa kura
6,173,433 dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga aliyekuwa na kura 5, 340,546
ikiwa ni tofauti ya kura 832,887 na majimbo yaliyo kwisha kutangazwa ni
291/291.
Jumla ya kura zote zilizopigwa na kuhesabiwa kwa nafasi ya Urais ni kura 12,338, 667 kutoka
katika majimbo yote ya Uchaguzi 291 huku kura zilizoharibika zikiwa 108975 na
kura halali zikibaki 12,222,980.
Katika kinyang’anyiro hicho Wycliffe Musalia
Mudavadi anashika nafasi ya tatu akiwa amejikusanyia kura 483,981 nafasi
ya nne ikienda kwa Peter Kenneth mwenye kura 72,786.
Mgombea wa Alliance for Real Change,Mohamud
Abduba Dida anashika nafasi ya tano akiwa na kura 52,848 akifuatiwa na
Mwana mama Martha Karua wa National Rainbow Coalition mwenye kura 43,881 hadi
sasa.
Nafasi ya saba katika wagombea hao Urais
inakwenda kwa James ole Kiyiapi wa Chama cha Restore and Build Kenya ambaye ana
kura 40,998 huku nafasi ya ya nane na mwisho ikishikwa na Paul Kibugi Muite wa
chama cha Safina.
Matokeo hayo yatatangazwa rasmi leo saa 5
asubuhi
0 comments:
Post a Comment