Mke wa rais mama Salma
Kikwete akisaidiana na Meneja miradi wa SBL Nandi Mwiyombela wakimtwisha ndoo ya maji mkazi wa jiji la Mwanza Getrude
Ngonyani kuashiria kuanza kutumika kwa kisima kwa ajili ya wakazi wa Mwanza.
Meneja miradi wa Kampuni
ya Bia ya Serengeti(SBL) Nandi Mwiyombela akitoa maelezo kwa mke wa Rais mama
Salma Kikwetejuu ya kisima kilichojengwa kwa msaada wa Kampuni ya Bia ya
Serengeti katika Hospitali ya mkoa wa
Mwanza - Sekou Toure
Meneja miradi wa Kampuni
ya Bia ya Serengeti Nandi Mwiyombela katikati akisalimiana na mke wa rais mama
Salma Kikwete mara baada yakuwasili katika hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekou
Toure kwaajili ya uzinduzi wa kisima cha
maji na pembeni yake ni Meneja mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mwanza
Patrick Kisaka
Mke wa Rais mama Salma
Kikwete akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi wa kisima kilichojengwa kwa
ufadhili wa Kampuni ya Bia ya Serengeti kwa ajili ya wakazi zaidi ya 160,000
waishio jijini Mwanza, kushoto kwake ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu na kaimu mkuu wa
mkoa wa Mwanza Pascal K. Mabiti na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya
Bia ya Serengeti (SBL) Jaji Mark Bomani.
**** ****
Kampuni ya Bia ya
Serengeti Breweries kupitia mpango wake wa kuisaidia jamii leo imekabidhi rasmi
mradi wa maji uliopo katika Hospitali ya Sekou Toure jijini Mwanza. Mradi huo
ulikabidhiwa na Mke wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma
Kikwete, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika makabidhiano hayo.
Mradi huo wa maji unatarajia kukidhi mahitaji ya
watu zaidi ya 160,000 waishio jijini Mwanza na ambao wanatibiwa au kufika
hospitalini ya Sekou Toure. Mradi huu
kwa kiasi kikubwa utapunguza mfumuko wa magonjwa na vilevile vifo vya watoto na
kina mama wajawazito. Mradi huu wa Hospitali ya Sekou Toure unajumuisha kisima
, pampu ya maji ya umeme na tanki la kuhifadhia maji la lita elfu kumi.
Kampuni ya Bia ya
Serengeti imetumia kiasi cha shilingi milioni 70 kukamilisha mradi huu. Kisima
hiki kina uwezo wa kutoa lita 240,000
kwa siku.
Akiongea katika
hafla ya makabidhiano hospitalini Sekou Toure , Mama Salma alisema
“ Nafarijika sana kujua kwamba Hospitali hii sasa imepata suluhisho la tatizo
la maji walilokuwa nalo hapo awali.Na napenda kuwashukuru sana Kampuni ya Bia
ya Serengeti kwa juhudi zao katika kusaidia shughuli za kijamii na hasa katika
upatikanaji wa maji safi na salama na hasa katika hospitali zetu.”
Kampuni ya Bia ya
Serengeti wamekuwa mstari wa mbele katika kusaidia upatikanaji wa maji safi na
salama na tayari wamewezesha miradi mbalimbali ya maji katika maeneo mbalimbali hapa nchini kama
vile Iringa – Hospitali ya Frelimo, Moshi – Hospitali ya Mawenzi , Dar-es
salaam – Hospitali ya Temeke na ule wa Mkuranga.
Mkurugenzi wa Mahusiano
na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti , Bwana Evans Mlelwa , amesema
“Suala la kuisaidia jamii kwa Kampuni ya Bia ya Serengeti limepewa kipaumbele
na uzito wa hali ya juu na hasa katika kusaidia upatikanaji wa maji safi ,
salama na pia endelevu.
Kama Kampuni SBL
inatambua umuhimu wa maji kwa binadamu na pia mchango wa maji katika maendeleo
ya nchi , kiuchumi na kijamii.Kama Kampuni kutafuta na kupata suluhisho la
kudumu ni katika kuhakikisha tunatoa msaada kwa jamii inayotuzunguka na
tunakofanya uzalishaji”. Aliongeza Mlelwa “Kampuni ya Bia ya Serengeti na EABL
Foundation mpaka sasa tumeshawekeza zaidi ya milioni 300 za kitanzania , katika
maeneo mbalimbali ambapo zaidi ya watu 450,000 wanafaidika na miradi hiyo”.
0 comments:
Post a Comment