Nafasi Ya Matangazo

February 20, 2013

 Jengo la Kisasa la Palace Hotel ambalo limefunguliwa leo na Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.



WAJASIRIAMALI nchini, wametakiwa kujitokeza katika ujenzi wa hoteli za kitalii nchini, ili kukabiliana na tatizo kubwa la uhaba wa vitanda katika hoteli za kitalii ambao unalikabili Taifa.

Naibu waziri wa Maliasilia na Utalii, Lazaro Nyarandu, alitoa wito huo jana wakati wa uzinduzi wa hoteli ya kitalii ya Palace Hoteli, ambayo imejengwa kwa ubia na Shirika la nyumba nchini(NHC).

Lazaro alisema uwekezaji huo utasadia kuongeza idadi kubwa ya watalii na  mapato,”mwaka jana tulipata watalii 800,000 ukilinganisha na  nchi ya Rwanda na udogo wake ilipata wageni 600,000 tatizo kubwa la nchi yetu ni upungufu wa vyumba vya kulala wageni”alisema.


Alisema mkakati huo utaufanya mkoa wa Arusha ambao ni kitovu cha utalii kuzidi kuongeza idadi ya vitanda vya kisasa kulala wageni  ambapo kwa sasa ina vitanda 2,800  tu nyuma ya mkoa wa Dar es salaam wenye vitanda 3,800 na kuzidi mkoa wa Mwanza wenye vitanda 900 licha ya ukubwa wake.

“Tunaomba shirika la nyumba lijitanue hadi maeneo hasa ujenzi wa hoteli za kisasa za kitalii…na sisi wizara tunahitaji wawekezaji wa ndani na nje kujitokeza kujenga katika maeneo ya wazi na ndani ya hifadhi zetu panapofaa…na tumejipanga kukabiliana na watumishi wenye urasimu wanaokwamisha watu wenye nia njema”alisisitiza.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu  alisema ujenzi wa hoteli hiyo yenye hadhi ya nyota nne, umegharimu kiasi cha sh 16 bilioni ambapo NHC imetoa ardhi n ash 9 bilioni huku kiasi kingine kikitolewa na Palace Hoteli.

Alisema mradi wa hoteli hiyo ni moja ya miradi ambayo imekuwa na manufaa makubwa, kutokana na uwazi katika uendeshwaji wake na hivyo kuingiza mapato kwa pande zote NHC na Mbia.

“binafsi nampongeza sana Mkurugenzi wa Palace hoteli, Dk Hans Macha kwa uwazi katika uendeshwaji wa mradi huu na tunamkaribisha katika miradi mingine aje tushirikiane”alisema Mchechu.

Naye Dk Ha Macha alisema mradi huo hadi sasa imetoa ajira ya wafanyakazi 120 na unatoa huduma nyingine kadhaa, ikiwepo huduma za kibenki na utachangia kwa kiasi kikubwa kikuza uchumi wa mkoa wa Arusha na Taifa.

“hoteli hii tunatumia malighafi za hapa Arusha toka kwa wajasiriamali ikiwa ni njia ya kuongeza ajira na kipato na pia tumekuwa na miradi mbali mbali ikiwepo na utunzwaji wa mazingira”alisema Macha.

Akifungua mradi huo rasmi, Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alipongeza mradi huo na kutoa wito kwa wajasiriamali wengine kujitokeza na kuingia ubia na NHC katika kutekeleza miradi mbali mbali.

Alisema mradi huo unakwenda vizuri na umeongeza mapato ya NHC kwani katika eneo hilo, kabla ya ujenzi wa hoteli walikuwa wakipata kwa mwaka kiasi cha sh 31 milioni pekee lakini sasa wanapata 151 milioni.

“natoa agizo rasmi kwa wabia wengine walioingia mikataba na NHC kama huu, kama hawajatekeleza hadi sasa basi mikataba yao ifutwe kwani ni hasara kwa shirika la Taifa”alisema Profesa Tibaijuka.

Posted by MROKI On Wednesday, February 20, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo