Nafasi Ya Matangazo

February 07, 2013

Meneja Mawasilianao wa Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa (kushoto) akimkabidhi fedha kiasi cha shilingi Milioni 5  mshindi  wa  Promosheni ya "MAHELA"Ofisa wa Polisi kanda maalumu ya jijini Dar es Salaam Bi.Liberata Kaligita.Aliejishindia kwenye promosheni hiyo inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,zaidi ya shilingi milioni 400 zinaendelea kushindaniwa,katikati ni Ofisa Polisi Bethuel Sumari.
Meneja Mawasilianao wa Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa (kushoto) akimsisitiza jambo mshindi wa Promosheni ya"MAHELA"ambaeni dereva wa Bajaji Mbezi Kimara Bw.Paskal Susuma(kulia)wakati wa kumkabidhi  pesa zake kiasi cha shilingi Milioni 1 aliyojishindia katika  promosheni hiyo inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,zaidi ya shilingi milioni 400 zinaendelea kushindaniwa,katikati ni Meneja uhusiano wa kampuni hiyo Bw.Matina Nkurlu.
*****
 
Promosheni ya MAHELA inayoendeshwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, imeendelea kusisimua hisia za watanzania kwa washindi zaidi kuendelea kupatikana na wakati huu bahati ikiwaangukia  Askari wa Jeshi la Polisi kanda maalumu Dar es Salaam Bi.Liberata Kaligita na Dereva wa  Bajaji ambae anaendesha bajaji za Mbezi Kimara Bw.Paskal Susuma.

Akizungumza wakati wa droo na makabidhiano ya pesa zao  na Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania katika makao Makuu ya kampuni  hiyo  yaliyoko Mlimani City jijini Dar es Salaam,Bi. Liberata Kaligita ambae ni mkazi wa Galax Barabara ya Kilwa amesema kuwa mara kadhaa alipokuwa akishiriki katika Promosheni hiyo Askari wenzake walimcheka sana lakini leo hii wataamini kuwa Vodacom Tanzania kupitia promosheni yake hii ya"MAHELA"hawana longolongo.

Kazi ni kwao kwa kujibu maswali kwa ufasaa tu,Kwa upande wake Mshindi wa pili wa Milioni moja ambaye amepatikana kutoka kwa washindi walioshiriki mara nyingi katika Promosheni hiyo amesema kuwa kamwe hakukata tamaa kushiriki katika promosheni hiyo kwa kujua kuwa ipo siku bahati itaangukia kwake na hakuweza kuizuia furaha yake kama ilivyokuwa katika Mazungumzo na kuongeza kwa kusema kwasababu yeye ni dereva wa bajaji anaipenda kazi yake lakini atafungua biashara ya M-pesa kwani Vodacom imemwezesha kupitia promosheni hii ya MAHELA.
Posted by MROKI On Thursday, February 07, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo