Wadhamini wa Timu ya Taifa (Taifa Stars),
Kilimanjaro Premium lager, wamesema wanarishishwa na kiwango cha timu hiyo kwa
sasa huku wakiomba TFF iandae mechi nyingi za Staridi za kirafiki hapa
nyumbani.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa Bia ya
Kilimanajro Premium Lager, George Kavishe siku moja baada ya Stars kuicharaza
Cameroon bao 1-0 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa katika Uwanja wa Taimu
hiiifa Jijini Dar es Salaam.
“Kwa kweli tunafurahishwa na mafanikio ya timu
hii tangu tuchukue udhamini mwezi Mei mwaka jana….tumeiangalia ikicheza ndani
na nje na kwa kweli kikosi ni kizuri kwani kimewaletea watanzania ushindi,”
alisema.
Aliwapongeza watanzania kwa kujitokeza kwa wingi
kuishangilia timu yao kama kauli mbiu ya KIlimanajro Premium Lager
inavyosema…”Sherekea kilicho chetu.
“Hawa walikuwa wanajulikana kama Simba wa Afrika
lakini wameondoka wakiwa wamenyong’onyea baada ya kufungwa 1-0,” alisema.
Bw Kavishe alisema ushindi huu wa Stars umewapa
nafasi nzuri ya kuendelea kuidhamini Taifa Stars ili kuwapa watanzania nafasi
ya kusherekea kilicho chao kwa kupitia burudani ya mpira.
“Dhidi watanzania wanavyozidi kutuunga mkono kwa
kunywa bia yetu ya Kilimanajro Premium Lager ndio sisi tunazidi kupata fedha za
kuidhamini timu na kuendelea kuwapa burudani ya mpira,” alisema Kavishe.
Alisisitiza kuwa TFF inatakiwa kuandaa mechi
nyingi za kirafiki hapa nyumbani ili watanzania wazidi kuiona timu yao
ikicheza.
Huu ni ushindi mnono wa pili mfululizo kwa timu
ya Taifa baada ya kuichapa Zambia 1-0 Disemba mwaka jana.
Kilimanjaro Premium Lager imetoa udhamini wa
zaidi ya Shilingi Bilioni 10 kwa miaka mitano. Huu ndio udhamini mkubwa kabisa
wa mpira ambao umewahi kutokea Tanzania.
0 comments:
Post a Comment