Meneja huduma kwa
wateja wa Airtel Hawa Bayumi akimkabithi Afisa elimu wa mkoa wa Mwanza
Hamisi Maulidi msaada wa vitabu kwa shule tatu za sekondari za Kalebezo,
Buhongwa, and Kabuhoro zilizopo mkoani Mwanza. wakishuhudia kulia ni
Meneja Mauzo wa Kanda Ally Maswanya na Meneja huduma ya Airtel money wa
Kanda Galus Mgawe.
Afisa
elimu wa mkoa wa Mwanza Hamisi Maulidi akipokea msaada wa vitabu
kutoka kwa Meneja huduma kwa wateja wa Airtel Hawa Bayumi
zilivyokabithiwa na Airtel chini ya mradi wake wa Shule yetu, shule 3
za sekondari za Kalebezo, Buhongwa na Kabuhoro za mkoani Mwanza
zilifaidika na Msaada huo.
**** ****
· Airtel yachangi vitabu vya sayansi kwa shule 3 za sekondari mkoani Mwanza
Wakati
Tanzania ikikabiliwa na uhaba wa wataalamu wa fani ya sayansi,wanafunzi
wametakiwa kutohofia masomo ya sayansi na kukimbilia kusoma masomo
mengine kwa lengo la kulifanya taifa liwe na wataalamu wengi wa fani
mbalimbali.Kauli hiyo imetolewa jijini Mwanza na Afisa Elimu wa Mkoa wa
Mwanza Hamis Maulid wakati akikabidhi vitabu kwa shule nne za sekondari
za mkoa huo vilivyotelewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.
Afisa
Elimu wa mkoa wa mwanza ameendelea kwa kusema elimu ni urithi endelevu
na kusoma masomo ya sayansi kunamwezesha mwanafunzi kuwa katika nafasi
nzuri ya kulisaidia taifa katika Nyanja ya kitaalamu. mataifa mengi
duniani yamepiga hatua kutokana na wanafunzi kupewa msukumo wa kusoma
masomo ya mchepuo wa sayansi.
Akiongea
katika halfa ya makabithiano ya vitabu mkoani Mwanza, Meneja wa huduma
kwa jamii wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Hawa Bayumi amesema
Airtel imeguswa na tatizo la ukosefu wa vitabu mashuleni na kusababisha
kiwango cha ufaulu kushuka hasa katika masomo ya sayansi. Na leo
tunayofuraha kutoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari za mkoa wa
mwanza zikiwemo: Kalebezo sekondari iliyopo wilayani Sengerema, shule
ya sekondari ya Buhongwa na Kabuhoro sekondari.
Tunaamini
mchango huu wa vitabu mashule utakuwa chachu ya maendeleo ya elimu
nchini na kuongeza kiwango cha ufaulu nchini. Tunaahidi kuendelea
kushirikiana na serikali chini ya wizara ya elimu katika kuhakikisha
tunafikia malengo waliojiwekea. Aliongeza Bayumi.
Naye
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Kalebezo iliyopo wilayani
Sengerema Thomas Muswaga na mwanafuzi Julieth John wa kidato cha nne
katika shule ya sekondari ya Buhongwa wanazungumzia changamoto
mbalimbali zikiwemo uhaba wa vitabu na kushukuru Airtel kwa msaada wa
vitabu walioutoa katika shule hizo za mkoa wa Mwanza
Airtel
chini ya mpango wake wa shule yetu imeendelea kutoa msaada wa vitabu
kwa shule za sekondari mbalimbali nchini. kwa mwaka huu shule 93 za
sekondari tangu kuanzishwa kwa mradi huo shule zaidi ya shule za
sekondari 900 zimekabithiwa
0 comments:
Post a Comment