Mgeni
Rasmi katika Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya (NHIF),Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt.
Seif Rashid akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano hilo
linalofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya
Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.Kauli mbiu ya Kongamano hilo kwa mwaka huu
ni “Matumizi Sahihi ya Fedha za Uchangiaji Katika Halmashauri ili
kuboresha huduma katika vituo vya matibabu”.
Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya ambaye ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa yote Nchini,Mh.
Abbas Kandoro akitoa salamu kwa Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya (NHIF) wanaoshiriki Kongamano hilo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Emmanuel Humba akitoa
taarifa fupi ya Mfuko wa Bima ya Afya kutokana tafiti mbali mbali
zilizofanywa na baadhi ya Wanahabari katika Halmashauri 26 hapa nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara mjini,Mh. Wilman Kapenjama Ndile akisalimia.
Wakijadiliana jambo.
Katibu
Mkuu wa Jukwaa la Wahariri wa vyombo vya Habari hapa nchini,Nevile
Meena akizungumza machache wakati wa Kongamano hilo la nane la
Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,linaloendelea hivi
sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu
Mkoani Mtwara.
Mkurugenzi
wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Raphael
Mwamotto akitoa muongozo na utambulisho kwa baadhi ya viongozi kutoka
sehemu mbali mbali wanaohudhulia Kongamano hilo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Eugin Mikongoti akiwasilisha mada yake kwenye Kongamano la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Wadau wakifatilia Mada zinazotolewa kwenye Kongamano hilo.
Wadau.
Mkuu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF),Athuman Rehani akiweka sawa mambo kabla ya kuwasilisha mada yake.
Baadhi
ya Wanahabari kutoka Vyombo mbali mbali vya Habari wakifatilia kwa
makini Kongamano hilo la nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa
wa Bima ya Afya (NHIF),linalofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin
Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.Picha na Othman Michuzi
0 comments:
Post a Comment