Nafasi Ya Matangazo

February 07, 2013

 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (wa pili kulia) akiwa amembeba mtoto Consolatha kwenye shule ya awali ya Kijiji cha Matumaini kinacholea watoto yatima eneo la Kisasa, Dodoma leo mchana Februari 7, 2013. Kulia ni Mwenyekiti wa UWT, wilaya ya Dodoma Mjini, Bi. Fatuma Mwenda na (kushoto) ni Mwenyekiti wa UWT Mkoa huo, Bi Salome Kiwaya.
 
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akiwa amembeba mtoto wa kiume aliyezaliwa leo saa 11 alfajiri (Februari 7, 2013) na Bi. Fatma Mohammed kwenye kituo cha afya cha Kijiji cha Matumaini. Mama wa mtoto huyo, Bi. Fatma Mohammed alisema atamwita mtoto huyo Pinda kwa sababu Mama Pinda amekuwa mtu wa kwanza kumjulia hali.

Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (kulia) akiwa amembeba mtoto Cyprian (doto) mmojawapo wa mapacha wanaolelewa katika kituo cha afya cha Kijiji cha Matumaini wakati alipotembelea kijiji hicho Februari 7, 2013. Pacha mwingine (kulwa) Christian)  amebebwa na Mwenyekiti wa UWT, Mkoa wa Dodoma, Bi Salome Kiwaya.  Kushoto ni Pd. Vincent Boselli akielezea jinsi watoto hao wenye miezi mitatu walivyofikishwa kituoni hapo wakitokea Morogoro.
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda (kulia) akiwa amembeba mtoto Elizabeth (mwenye miezi saba) anayelelewa katika kituo cha afya cha Kijiji cha Matumaini wakati alipotembelea kijiji hicho Februari 7, 2013.
Baadhi ya watoto wa Kijiji cha Matumaini wakiangalia zawadi walizopelekewa leo Februari 7, 2013 na Mama Tunu Pinda wakati alipotembelea kijiji hicho.

Neema Ntandu (wa tatu kushoto) ambaye ni mmojawapo wa watoto watatu waliokuwepo wakati Kijiji cha Matumaini kikianzishwa mwaka 2002, akimkabidhi zawadi ya sanamu ya Bikira Maria, Mama Tunu Pinda ambayo imetengenezwa na watoto wa kijiji hicho wakati Mama Pinda alipotembelea kijiji hicho leo mchana, Februari 7, 2013. Picha na Irene Bwire – OWM.
Posted by MROKI On Thursday, February 07, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo