Nafasi Ya Matangazo

February 07, 2013

RAIS wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete amehaidi kuwasaidia Mamlaka ya   Vitambulisho (NIDA)  kwa kuiwezesha  kupata fedha  kwa ajili  Vitambulisho vya Taifa  ili  kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 watu wote watakuwa na vitambulisho vya Taifa vitakavyo tumika katika uchaguzi huo.
 
Aidha  Rais  Kikwete  aliitaka NIDA  kutoa vitambulisho kwa watu wanaotakiwa na kuchukulia hatua za kisheria wale  watakaokiuka sheria ya usajili wa vitambulisho hivyo.
 
Kauli hiyo ilitolewa  leo na Rais Kikwete wakati uzinduzi wa mfumo wa usajili na utambuzi wa watu kitaifa na utoaji wa vitambulisho hivyo  uliofanyika  katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
 
Rais Kikwete aliwataka wananchi kuwa wazalendo kwa  kutoa taarifa zao kwa uaminifu na kutoa ushirikiano ili kurahisisha  zoezi hilo.
 
Aliwataka viongozi wa dini, serikali na waandishi wa habari kuwa mstari wa mbele katika kuwahamasisha wananchi kutoa ushirikiano huo.
 
Naye Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi  Dk. Emmanuel  Nchimbi alisema ni  muhimu kuwa na vitambulisho vya Taifa kwani ni jambo la msingi ambalo litaweza kuwa na manufaa makubwa kwa kuunganisha mifumo mikubwa ya usajili ya kitaifa.
 
Baadhi ya mifumo hiyo ni kama Mfumo wa usajili wa kodi(TRA), Mfumo wa vizazi na vifo(RITA),Mfumo wa pasi za kusafiria(UHAMIAJI),Mfumo wa POLISI, Mifumo ya mawasiliano ya simu(Vodacom,Tigo,Zantel,Airtel,TTCL),Mfumo wa Taarifa za kiutumishi na Mishahara Serikalini, Mifumo ya Hifadhi za kijamii,Mifumo ya Taasisi za kifedha,Mifumo ya udahili ya Wanafunzi(Loan Board),n.k.

 
Mkurugezi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu alizitaja changamoto mbalimbali za kiutendaji zikiwemo wananchi kukosa viambatanisho muhimu vya kuwatambulisha,uhakiki wa taarifa za uraia,Uhakiki wa taarifa za makazi,Upungufu wa vifaa na Rasilimali watu.
 
Aliyataja mahitaji halisi ya zoezi hilo kuwa ni  vifaa vya kuchukulia alama za vidole, picha saini  takribani 12,000, rasilimali watu wa muda 114,000 na wakudumu 3000 ili kukukamilisha  mpango huo kwa muda utaotakiwa.
Posted by MROKI On Thursday, February 07, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo