Mkurugenzi Mkuu wa
Alliance One Tobacco Tanzania Ltd. (AOTTL) Bw. Mark Mason
Mwandishi:
Mara zote watu wakisikiapo Alliance One Tobacco Tanzania wanadhania ni kampuni inayozalisha
sigara, ambayo si kweli; je Alliance One inajishughulisha na nini hasa?
Mark Mason: Alliance One Tobacco Tanzania (AOTTL) ni moja kati ya makampuni matatu
yanayonunua bidhaa ya tumbaku nchini Tanzania iliyo chini ya mwamvuli ya
kampuni ya kimataifa Alliance One International (AOI) yenye makao makuu North
Carolina, nchini Marekani. AOTTL ilianza kazi nchini Tanzania mwaka 2005 baada
ya kuunganishwa kwa makampuni ya kimataifa DIMON Incorporated na Standard
Commercial Corporation (STANCOM) zote kutoka Marekani.
Shughuli inayofanya Alliance One
Tobacco Tanzania ni kununua tumbaku, kuiandaa kiwandani na kuiuza ndani na nje
ya nchi kwa makampuni yanoyotengeneza sigara. AOTTL inanunua kati ya kilo
milioni 30 mpaka 50 za tumbaku kutoka kwa wakulima 182 waliokuwa na mikataba na
Shirika la Wakulima wadogo wadogo kutoka sehemu 8 tofauti zinazolima tumbaku
nchini Tanzania ikiwemo Tabora, Urambo, Kahama, Manyoni, Iringa, Kigoma, Songea
na Mara. AOTTL inazalisha aina mbili za tumbaku zenye majina yakitaalam Flue
Cured Virgina (FCV) na Dark Fire Cured (DFC).
Mwandishi: Ni kitu gani kinachofanya Tanzania iwe na
mazingira bora ya kufanya biashara tofauti na nchi zingine?
Mark Mason: Uwekezaji
mkubwa wa kampuni yetu nchini Tanzania ipo Kingolwira, Morogoro ambapo
tumewekeza dola za kimarekani milioni 50 sawa sawa ma bilioni 50 zakitanzania.
Kushamiri kwa uwekezaji huu wa Alliance One ni matokeo ya sera nzuri za
uwekezaji na mazingira bora yakufanya
biashara inayowezeshwa na serikali ya Tanzania kupitia Kituo cha Uwekezaji
Tanzania maarufu kama TIC.
Mwandishi: Hivi karibuni utafiti uliofanywa na taasisi ya
wanauchumi wakujitegemea NKC kwa dhamana ya taasisi ya Tumbaku kwa nchi za
kusini mwa Afrika (Tisa), imetangaza thamani ya sekta ya tumbaku kuwa dola bilioni
10 kwa kusini mwa jangwa ya sahara. Kampuni yenu inapokeaje taarifa hizi,
hususani wakati huu ambapo tume yakukumbana na tumbaku (FCTC) inafanya jitihada
ya kufungia kilimo na biashara ya tumbaku duniani?
Mark Mason: Alliance
One ilijishirikisha kikamilifu katika utafiti huu na inakaribisha kwa furaha
kubwa hizi taarifa kwa sababu ni mara ya kwanza kwa tafiti ya thamani ya
tumbaku kufanywa katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara. Utafiti huu wa
TISA inatusaidia kubadilishana mawazo kuhusu umuhimu wa sekta ya tumbaku, sio kwa jumla ya uchumi
wetu tu bali kwa nchi zinazo lima tumbaku pia. Matokeo ya utafiti huu yanaweza
kutumika na wadau mbali mbali kama serikali (kwa ajili yakutunga sera na
mipango), mamlaka za udhibiti, mamlaka za kukusanya mapato na watoa huduma
mbali mbali.
Kuhusiana na sera ya FCTC
kufungia tumbaku, utafiti huu utasaidia wadau mbali mbali wa FCTC wanaolima
tumbaku kuweka sera ambazo zitafanikisha maamuzi sahihi kwa ajili ya kulima
tumbaku.
Mwandishi: Je nini athari ya kusimamisha kilimo cha na
kuuza tumbaku kama FCTC itafanikiwa kupitisha sera hiyo?
Mark Mason: FCTC ikifanikiwa katika
kampeni yake ya kuzuia tumbaku duniani, athari zake katika uchumi wa Tanzania yatakuwa
kama yafuatayo; Maisha ya wakulima 100,000 na familia zao zitaathiriwa sana kwa
sababu hakuna zao mbadala uliopatikana mpaka sasa. Pili, kwa uchumi wa
Tanzania, fedha za kigeni kutokana na mauzo ya tumbaku yatasimama. Pia mapato
ya serikali kutokana na tumbaku na bidhaa za tumbaku yanayokadiriwa kuwa
shilingi bilioni 157 nazo zitayumba. Hii ni kwa sababu katika miaka mitatu
iliyopita tumbaku ndio imekuwa ikiongoza katika zao linalopatisha nchi yetu
fedha za kigeni kwa kusafirishwa nje.
Kutokana na takwimu za Benki Kuu ya Tanzania katika ripoti
ya Septemba 2012, mauzo ya tumbaku nje ya nchi kufikia Agosti 2012 yalifikia
dola milioni 307.3. Maisha na maendeleo ya wafanyakazi na wategemezi takribani
790,000 sawa sawa na asilimia 1.5 ya idadi ya watu ambao wananufaika moja kwa
moja na kutegemea mlolongo wa thamani na mapato ya zao la tumbaku nao
wataathirika.
Mwandishi: Kama FCTC wapo sahihi, je kuna uwezekano
wakupata mbadala wa zao la tumbaku kama zao la biashara linaloongoza kwa kuuzwa
nje ya nchi Tanzania?
Mark Mason: Mpaka sasa
kumekuwa na mazao mbadala machache sana zinazotajwa na kuhakikishwa kuweza kuchukua
nafasi yakulimwa katika mashamba ya tumbaku yaliyopo sasa. Mapendekezo
yameshatolewa kwa sektretarieti ya FCTC
na wadau wa tumbaku kuwa utafiti zaidi juu ya mazao mbadala yanabidi
yafanyike.
Mwaandishi: Inavyoonekana, watu wengi wanafahamu athari za kiafya
zaidi zinazoletwa na tumbaku kuliko manufaa inayoleta kiuchumi, je unadhani
elimu imetolewa vya kutosha ili watu waweze kuelewa mchango wa zao hili kiuchumi
katika taifa letu?
Mark Mason: Ndio, jitihada
zimefanyika kujaribu kuwafahamisha watu kuhusiana na manufaa ya tumbaku katika
uchumi wetu kupitia vyombo vya habari, warsha na mikutano mbali mbali. Kwa
mfano, mwaka 2012 Alliance One ilifanya mkutano na wahariri wa vyombo vya
habari kuhusiana mambo kadha wa kadha ya sekta hii ikiwemo umuhimu wa tumbaku
katika uchumi wa Tanzania.
Mwandishi: Inavyoonekana, wakulima wa tumbaku ndio wadau
wakubwa wa Alliance One, je mnawejengea vipi mazingira bora ya kazi kwenye
kilimo na kupata masoko ya mazao yao?
Mark Mason: Alliance
One imeingia mkataba wa miaka mitatu yakununua tumbaku kutoka kwa wakulima
waliojiunga na mashirika ya wakulima wadogo wadogo. Kupitia mikataba hii
wakulima wana uhakika wa kupata soko la tumbaku yao. Alliance One inawapatia
huduma mbali mbali pia wakulima hawa ikiwemo; Mikopo kwa waakulima kupitia
mikataba ya mikopo na benki zinazokopesha inayohakikiashia benki marejesho ya
mkopo kwa sababu mkulima anakuwa ana uhakika na kuuza tumbaku yake kutokana na
soko la Alliance One. Alliance One pia inatoa huduma za kuandaa mipango ya
mauzo na masoko kwa wakulima na uratibu huo kupitia wakala wake anayitwa asasi
ya wafanyabiashara wa tumbaku Tanzania (ATTT).
Pia, Wadau wa tumbaku kupitia
baraza la tumbaku pia wameanzisha mkakati mpya wa kitaifa wa kupanda miti
inayozingatia mkulima kutumia miti kwa nidhamu kwa ajili ya kuandaa tumbaku na
matumizi ya nyumbani kuanzia msimu 2012/2013. Kupitia mpango huu, wakulima
watahitajika kupanda miti katika mashamba yao na kutakuwa na ukaguzi kila mwaka
na kutegemeana na matokeo ya ukaguzi, Alliance One itarudisha gharama zote za
mbegu, kupanda na kuotesha miti.
Mwandishi: Umesema kampuni yako imekuwa ikifanya kazi kwa
muda sasa nchini Tanzania. Je ni faida gani kubwa iliyoiletea jamii ya
watanzania mpaka sasa?
Mark Mason: Kama
nilivyotamka mwanzo, biashara ya AOTTL nchini Tanzania ni ya kununua tumbaku,
kuiandaa kiwandani na kuiuza. Kwa kufanya haya, biashara ya AOTTL inafaida
mbali mbali katika jamii ya watanzania kama ifuatavyo; Uwezeshwaji wakiuchumi
wa wakulima wapatao 38,000 pamoa na familia na jamii inayowazunguka katika
mahali wanapolimia. Pili, kutoa ajira kwa watanzania wapatao 300 kama waajiriwa
kamili na 2,500 kama vibarua wakati wa misimu ya kilimo. Tatu, AOTTL pia
imeweza kusambaza aina ya teknolojia kwa wakulima iliyowawezesha kuongeza
mavuno kutoka kilo 1060 kwa hekari moja 2005 mpaka kilo 1390 mwaka 2012. La
mwisho, kupitia malipo yetu ya kodi baraza la wilaya, serikali za mikoa na
serikali kuu zimeweza pia kutoa huduma za kijamii kama elimu, maji na afya,
pamoja na kuboresha hadhi ya miundombinu kama barabara.
Mwandishi: Mbali na kutoa nafasi za ajira na kuwawezesha
watu kiuchumi, je kuna mkakati wowote wa misaada kwa jamii mliowahi kutoa?
Mark Mason: AOTTL imejikita kuboresha hali ya maisha ya jamii za
wakulima wa tumbaku kupitia mpango maalum wa kutoa misaada inayolenga katika
elimu, afya na maendeleo ya kijamii. Kila mwaka AOTTL inatoa bajeti ya dola
laki moja na ishirini sawia na shilingi milioni 192 ambayo inagawiwa kwa watu
au vikundi vya maendeleo wanaotuomba misaada hii kupitia barua rasmi
zinazopitiwa na kamati husika na kutolewa kwa njia ya vitu. Baadhi ya misaada
ambayo tumejikita nayo ni kujenga madarasa, kugawa madawati, kutoa vitabu na
kulipia karo za wanafunzi wanohitaji msaada. Pia tunajenga kliniki na
kuwasaidia watoto yatima.
Pamoja na hayo, mpango wetu wa
kutoa msaada pia inaambatana na programu maalum ya wafanyakazi katika kilimo
yenye malengo mbali mbali katika sekta ya utendaji kazi wa kilimo cha tumbaku
kama ifuatazo; kufuta utumikwishaji wa watoto katika kilimo, kulinda maslahi ya
mapata na masaa ya kazi kwa mfanyakazi, kupatiwa mazingira salama ya kazi, kushirikishwa
kwa haki katika shughuli za kilimo, kufutwa kwa utendaji kazi wa kulazimishwa
yaani “Forced labour”, kuwajengea uhuru
wa kujiunga na mashirika ama asasi za kilimo na tumbaku na mwisho ni kuhakikisha
sheria za kazi zinafuatwa.
Mwandishi: Je, Alliance One inamipango gani ya baadae nchini
Tanzania?
Mark Mason: Sekta ya
tumbaku nchini Tanzania inategemewa kuwa na mwonekano mzuri sana mbele ya
safari kwa sababu tutabakia kuwa
washindani imara na kuendelea kuboresha maslahi kwa wakulima. Kwahiyo mipango
yetu ya baadaye inajumuisha; kuendeleza kukuza kwa nafasi ya Tanzania katika
soko la duniani huku tukizingatia gharama na ubora tukijilinganisah na nchi
zingine, kuendelea kuimarisha maisha ya wakulima, kuendelea kuwekeza katika
sehemu za masoko ili kuweza kumnufaisha mkulima kwa kumpunguzia siku za kufanya
kazi zinazotakiwa kuzalisha mazao, pamoja na kuongeza namna bora ya uzalishaji
na kufuta vitendo haramu katika kilimo tuikizingatia sheria za kazi, kuongeza
uwekezaji katika kiwanda na ufanisi ili kuweza kuwasaidia wakulima katika kilimo
cha tumbaku na kupunguza gharama kubwa katika zoezi la kupanda miti na hatimaye
kuendelea kuuza tumbaku iliyobora na kwa bei yenye ushindani ili kuweza kupata
mwendelezo wa masoko duniani.
0 comments:
Post a Comment