Dar
es Salaam, Tanzania - Februari 4, 2013- Ecobank Tanzania ambayo ni mojawapo ya
benki katika kundi la Ecobank Africa iliyo katika nchi 33 Africa, inazidi kukuza uwezo
wa wanabiashara Tanzania katika kushiriki biashara kati ya Tanzania na
China kwa kupunguza garama za uendeshaji biashara kati ya nchi hizi.
Wakishiriki katika
sherehe ya mwaka mpya ya China Jumapili hii katika viwanja vya Mnazi Mmoja,
Ecobank ilionyesha nia yake ya kusaidia jamii ya waendesha biashara kati ya
Tanzania na China zikiwepo huduma zinazorahisisha wafanyabiashara wa Tanzania
na wawekezaji wa Kichina kushiriki katika uagizaji na mauzo ya nje kati ya nchi
hizi. "Sisi tunayo nia ya kutoa huduma za garama nafuu na kurahisisha
upatikanaji wa bidhaa hizi kuwezesha sekta hii inayokua kwa kasi sana.
Katika mwongo
uliopita kumekuwa na uwekezaji wa $ 868 bilioni wa china ndani ya Tanzania,
huduma zetu zinajaza pengo la kurahisisha biashara hii "anasema Bw Enoch
Osei-Safo, Mkurugenzi Mtendaji Ecobank Tanzania.
Ecobank
inazindua huduma ya kubadilisha hela ya Tanzania kupata sarafu za kichina (RMB)
moja kwa moja, ambapo hapo awali hapa Tanzania, wanabiashara walilazimika
kubadili TZS kwa Dola za kimarekani ili kununua RMB. Katika mfumo huo wa awali,
wanabiashara walipoteza kiasi kikubwa cha mtaji lakini sasa, Ecobank
itatwawezesha wanabiashara kupunguza garama hizi kwa kueneza huduma hii hapa
Tanzania.
"
Sisi hatuwezi kupuuza matokeo ya biashara ya China juu ya Afrika, ambayo
inafikia zaidi ya dola bilioni 200 katika mwaka 2012 kwa uagizaji na 5% ya
mauzo yote ya Afrika kwenda nchini China, ushirikishwaji wa kifedha kukuza
sekta hii ni muhimu, na ndiyo maana Ecobank Group imeonyesha nia ya kurahisisha
uendeshaji wa biashara hii na kuwezesha Afrika kuwa na ushindani na nchi
zingine duniani.” Enoch aliongeza.
Ecobank
Tanzania katika miezi michache ijayo itakua kituo cha kutoa huduma za
uendeshaji biashara kati ya Tanzania na China kwa kutoa huduma ya ubadilishaji
wa sarafu ya kichina na pia kulipia kodi ya forodhani kwa TRA papo kwa papo
kupitia huduma ya Asybank katika matawi yote ya Ecobank.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akipata taarifa kutoka kwa Balozi wa China Nchini Tanzania
Lu Yuquing wakati wa sherehe hiyo iliyofanyika Dar es Salaam. Kulia kwa Waziri
Mkuu ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara,
na Kaimu Mkuu wa Mkoa, Pia Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi
0 comments:
Post a Comment