Bw.
William Mpinga Brand Manager wa Kampuni ya Tingo akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam juu ya Tamasha la muziki la
TABASAMU litakalofanyika kwenye fukwe za Coco Beach jijini Dar es
salaam mwezi huu.
Wasanii watakaoshiriki katika tamasha hilo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano wao.
****
Tigo Tanzania inapanga kufanya
tamasha kubwa la kuzindua msimu wa Tabasamu ambao umetokana na Tigo
kubadilisha kauli mbiu yake ya zamani kutoka Jielezee mwenyewe” kuwa
“Tabasamu! upo na Tigo”.
Meneja wa chapa ya Tigo
Bwana William Mpinga alielezea kuhusu uzinduzi huo akisema “Tigo ina
fahari kubwa kwa jinsi ambavyo inawajali na kuwapa thamani wateja wake
kupitia bidhaa zake mbalimbali za mawasiliano. Mabadiliko haya ya kauli
mbiu yanatupa fursa ya kuonyeshadhamira yetu ya kuwajali
Watanzania pamoja na kuwahakikishia kwamba tutakuwa nao sambamba kwa
kila jambo, wakati wote.
Wateja wetu ni msukumo wa kila tufanyacho Tigo,
hivyo tunajitahidi kuhakikisha tunawatimizia mahitaji yao yote ya
mawasiliano. Lengo letu linabakia kujenga na kutoa huduma za unafuu ,
zinazopatikana kila mahali na kwa wote.”
“Uzinduzi wa msimu huu wa Tabasamu
unalengo la kuhakikisha watu wengi zaidi wanatabasamu kutokana na
bidhaa zetu zenye thamani, mtandao wenye ubora wa juu na huduma nzuri
kwa wateja kama ishara ya shukrani kwa nafasi yetu muhimu kwenye maisha
ya Watanzania. Tumekuwa ni sehemu ya maisha yako na tunataka kuwa na
wewe siku zote hivyo Tabasamu, upo na Tigo! ” Alihitimisha Bwana Mpinga.
Tamasha hili litafanyika katika
ufukwe wa Coco (Coco Beach) Jumapili ya tarehe 10 Februari 2013 kutoka
saa 7:00 mchana hadi saa 12:00 jioni na litashirikisha burudani kali
kutoka kwa Enika, Roma Mkatoliki, TMK Wanaume, Tip Top Connection, Juma
Nature, Recho, Mr. Blue na wachezaji dansi wa THT .
Mtaalamu wa Biashara na Masoko wa
Tigo bwana Alex Msigara alisema juu ya tamasha kwamba “ukiachana na
burudani kutoka kwa wanamuziki hao mahiri vilevile kutakuwa na zawadi
kubwa za kushindaniwa na promosheni na ofa za kusisumua. Tutakuwa na
bidhaa na huduma mbalimbali za ofa za Tigo hivyo tunatarajia ujio mkubwa
na tunawahakikishia burudani kali ya kuanza mwaka na tabasamu”
Msimu huu wa tabasamu unahusisha
ofa, promosheni, zawadi na bidhaa mbalimbali za thamani kutoka Tigo
ambazo zitawalenga wateja wa vipengele vyote na mahitaji yao yote.
0 comments:
Post a Comment